Yajue matumizi sahihi ya Albendazole, dawa inayotumika kutibu minyoo. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, January 18, 2017

Yajue matumizi sahihi ya Albendazole, dawa inayotumika kutibu minyoo.

Dawa za kutibu minyoo ni dawa ambazo watu wengi mtaani wanazitumia bila hata ya kutafuta ushauri wa kitaalam. Watu wengi wakiona mtoto au mtu mzima anakula sana moja kwa moja hufikiria sababu itakuwa ni minyoo.


Mtu akiona anaumwa njaa sana siku hizi hufikiria tatizo litakuwa minyoo. Leo ningependa tufahamu matumizi sahii ya dawa hizi.

 Albendazole ni dawa inayotumika kutibu watu na wanyama wanaosumbuliwa na ugonjwa wa minyoo.

Albendazole ikitumika vizuri kama inavyotakiwa huua kabisa vimelea vyote (sensitive parasites). 

Usitumie Albendazole kama una aleji (allergy) na kiambato chochote kilichopo kwenye albendazole au benzimidazole (mfano, Rabeprazole). 

Wasiliana na wataalam wako wa afya kama chochote kati ya hivyo viwili hapo juu kinakuhusu.

Kabla ya Kutumia Albendazole;

Kuna hali mbalimbali za kiafya zinazoweza kuingiliana na albendazole. Wasiliana na daktari wako au mfamasia kama una hali hizi zifuatazo:

•            Kama ni mjamzito, unatarajia kuwa mjamzito au unanyonyesha
•            Kama una dawa nyingine yeyote ambayo unatumia, au dawa asili au dietary supplement yeyote

•            Kama una aleji(allergy) na dawa, chakula au kitu kingine chochote
•            Kama una matatizo ya ini, macho, mifupa au kupungukiwa dawa mara kwa mara.

Zifuatazo ni baadhi ya dawa zinazo ingiliana (interact) na albendazole :
•            Cimetidine, dexamethasone au praziquantel dawa hizi huangeza madhara (side effects) za albendazole.
•            Theophylline, madhara (side effects) ya dawa hii huongezeka endapo mtu atachanganya na albendazole.

Huu sio muingiliano pekee unaoweza kutokea kama mtu atatumia albendazole pamoja na dawa zingine. Upo muingiliano mwingi. Wasiliana na mtaalam wako wa afya kabla haujaanza, haujasimamisha au kubadili dozi ya dawa yako yeyote ile.

Matumizi Sahihi ya Albendazole

Tumia kama ulivyoelekezwa na daktari wako. Angalia kwenye lebo ya dawa yako kwa ajili ya maelezo zaidi.

•            Tumia kwa njia ya mdomo kama unashindwa kumeza kidonge kizima, unaweza kukitafuna kwanza kasha kumeza na maji kidogo.

•            Kama ukisahau kumeza dozi moja kwa muda muafaka, jitahidi kunywa kabla muda haujapita zaidi. Kama muda wa kunywa dozi nyingine umefika, endelea na dozi nyingine kama kawaida, usinywe dozi mbili kwa mara moja. Kama umesahau kunywa zaidi ya dozi moja, wasiliana na daktari au mfamasia wako.

•            Albendazole inaweza sababisha kizunguzungu. Madhara haya yanaweza kungezeka kama utatumia pombe na albendazole kwa wakati mmoja.

•            Albendazole inabidi zitumike kwa uangalifu mkubwa kwa watoto wa chini ya mwaka mmoja kutokana na kuwa usalama wa dawa hizi kwa kundi hili la watoto bado haujafhamika vizuri.

•            Usitumie albendazole kama una ujauzito au unanyonyesha. Albendazole zinaweza kusababisha madhara makubwa kwa mtoto aliyepo tumboni. Bado hakuna majibu ya moja kwa moja kama albendazole huteza kupenya na kuingia kwenye maziwa ya mama anenyonyesha. 

Na ikiwa utatumia dawa hii na unaujauzito wasiliana na daktari wako kwa ushauri zaidi.

Nitoe wito kwa Watanzania kuacha kutumia dawa holela bila ya kufuata ushauri wa kitaalamu.

Your Health, My Concern

IMEANDIKWA NA
FORD A. CHISANZA
Pharmacist
Scientist/Researcher at DawaCALL
Location: Off Mandela Road, Mabibo – External,
P.o.Box: 77150, Dar Es Salaam, Tanzania.
Mobile:+255 652466430/+255 684363584
Email: fordchisanza@gmail.com
fordchisanza@yahoo.com

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad