VPL 2016/2017: Yanga SC waisurubu Majimaji FC Mjini Songea. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, January 17, 2017

VPL 2016/2017: Yanga SC waisurubu Majimaji FC Mjini Songea.


Wachezaji wa timu ya Yanga SC wakishangilia ushindi dhidi ya timu ya Majimaji FC leo January 17, 2017 katika Uwanja wa Majimaji, Songea.   
Yanga SC wanaondoka na pointi 3 muhimu kwa kuichapa Majimaji  FC bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania bara 2016/2017 kwa Bao la ushindi lililopachikwa Dakika ya 14 na Deus Kaseke.



Matokeo haya yamewaweka Yanga SC kuwa Pointi 1 nyuma ya Vinara Simba SC ambao kesho Jumatano January 18, 2017 wapo huko Jamhuri Jijini Morogoro kucheza na Mtibwa Sugar.

Mechi nyingine ambayo pia itachezwa kesho ni huko Chamazi kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam kati ya Azam FC na Mbeya City.

MSIMAMO VPL 2016/2017.



1 Simba SC Mechi 18 Pointi 44



2 Young Africans Mechi 19  Pointi 43



3 Kagera Sugar   Mechi  19 Pointi 31



4 Azam FC          Mechi  18 Pointi 30



5 Mtibwa Sugar  Mechi 18 Pointi 30


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad