Wekundu wa
msimbazi –Simba SC, ambao ni Vinara wa Ligi Kuu Vodacom, Leo January 28,2017
Jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Taifa wamefungwa 1-0 na Azam FC na huko
Sokoine, Mbeya kwenye Dabi ya Mji huo, Tanzania Prisons imeifunga Mbeya City
2-0.
Kwa Simba SC
, hiki ni kipigo cha pili mfululizo toka kwa Azam FC ambao Januari 13,2017 waliichapa
Simba 1-0 na kubeba Kombe la Mapinduzi huko Amaan Stadium Zanzibar.
Kwenye Mechi
hiyo, Mfungaji alikuwa Himid Mao lakini Leo ni Kepteni wao John Bocco ndie
alifunga Bao 1 na la ushindi katika Dakika ya 70.
Matokeo haya
yameibakisha Simba SC kileleni mwa VPL 2016/2017 wakiwa na Pointi 45 kwa Mechi
20 na kufuata Yanga SC wenye Pointi 43 kwa Mechi 19 wakati Azam FC ni wa 3
wakiwa na Pointi 34 kwa Mechi 20.
Yanga SC
Kesho Jumapili January 29, 2017 wapo dimbani Uwanja wa Taifa Jijini Dar es
Salaam kucheza na Mwadui FC na ushindi kwao utawaweka kileleni.
Nako huko
Sokoine, Mbeya kwenye Dabi kati ya Tanzania Prisons imewachapa Mbeya City Bao
2-0 kwa Bao za Samatta na Asukile.
Jumatatu
Januari 30,2017.
Kagera Sugar
v Mtibwa Sugar
JKT Ruvu v
Stand United
|
No comments:
Post a Comment