Tuzo binafsi walizoshinda Wachezaji Mapinduzi Cup 2017. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, January 14, 2017

Tuzo binafsi walizoshinda Wachezaji Mapinduzi Cup 2017.

Mdau wa soka Raza Lee akikabidhi viatu na kombe dogo kwa Agrey Morris (Azam FC) ambaye alitangazwa kuwa man of the match wa mchezo wa fainali ya Mapinduzi Cup 2017
Baada ya mashindano ya Mapinduzi kufikia tamati Januari 13, 2017, Azam FC ndio Mapingwa wapya wa kombe hilo.
Mbali na timu zao kupata au kukosa Ubingwa wa taji la Mapinduzi, kuna wachezaji ambao wamejishindia zawadi/tuzo binafsi baada ya kumalizika kwa mashindano.

Tuzo zilizotolewa kwa wachezaji binafsi ni pamoja na;

Mfungaji boraSimon Msuva (Yanga SC ) magoli 8

Mchezaji bora kijana/chipukiziSaid Mohamed ‘Messi wa Unguja’ (Taifa Jan’ombe)

Mchezaji bora wa mashindanoMethod Mwanjale (Simba SC)

Golikipa bora wa mashindanoAishi Manula (Azam FC hajaruhusu goli kwenye mechi tano za mashindano.

Mwamuzi bora wa mashindano Mfaume Ali Narror

Kila mshindi wa tuzo binafsi amekabidhiwa kiasi cha shilingi milioni moja (1,000,0000) kama tuzo kutokana na umahiri waliouonesha kwenye mashindano ya mwaka 2017.

Agrey Morris (Azam FC) alitangazwa mchezaji bora wa mechi ya fainali. Mdau wa soka Raza Lee akamkabidhi viatu vya kuchezea mpira pamoja na kombe dogo kama tuzo kwa kufanikiwa kuwa man of the match.

Kuanzia hatua ya nusu fainali, Raza Lee alikuwa anatoa zawadi ya viatu kwa mchezaji anayetangazwa kuwa man of the match.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad