VIDEO: Rais Magufuli Akitoa ONYO Kali Kwa Magazeti. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, January 14, 2017

VIDEO: Rais Magufuli Akitoa ONYO Kali Kwa Magazeti.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Ijumaa Januari 13,2017 amefungua rasmi viwanda viwili mkoani Shinyanga.

Rais Magufuli amefungua Kiwanda cha kutengeneza vifungashio vya bidhaa mbalimbali ikiwemo mifuko ya Sandarusi cha Fresho Investment Company Limited na kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited kinachojihusisha na uzalishaji wa vinywaji baridi ikiwemo soda,juisi na maji.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameyaonya magazeti mawili yanayoandika habari za uchochezi na kupotosha wananchi kwa kuwa vinahatarisha amani ya nchini.

Ametoa onyo hilo jana wakati akikagua na kufungua Kiwanda cha Jambo cha kuzalisha vinywaji baridi mkoani Shinyanga.

Rais Magufuli alisema Serikali haitayavumilia magazeti hayo mawili kwa kuandika habari za uchochezi ambazo zinaweza kuhatarisha amani ya nchi kama ilivyotokea katika nchini ya Rwanda na kupelekea mauaji ya kimbari nchini humo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad