Azam FC Yatwaa taji la tatu la Kombe la Mapinduzi 2017. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, January 14, 2017

Azam FC Yatwaa taji la tatu la Kombe la Mapinduzi 2017.

Hatimaye timu ya Azam FC imefanikiwa kutwaa Ubingwa wa taji la Mapinduzi 2017 baada ya ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Simba SC kwenye mchezo wa fainali uliochezwa kwenye uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Bao safi la mchezaji, Himidi Mao akitikisa  nyavu kwa shuti kali akiwa nje ya box ndilo limeipa Azam FC kwa mara ya tatu wa kombe hilo.

Awali timu za Simba SC na Yanga SC zilipewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri kutokana na moto wao kwenye ligi kuu Tanzania bara huku Azam FC ikipewa nafasi ndogo kwa kuangalia rekodi zake kwenye ligi pamoja na kuondokewa na kocha wao siku za usoni.

Rekodi za Azam bada ya kuchukua ubingwa wa Mapinduzi 2017.

Azam FC ndiyo timu pekee ambayo haijaruhusu goli hata moja kwenye mashindano ya mwaka 2017.

Ubingwa wa mwaka 2017 unaifanya Azam FC kuifikisha mataji matatu na Simba SC kwa idadi mataji ya Mapinduzi tangu mwa 2007.

 Azam FC imechukua taji hilo mwaka 2012, 2013 na 2017.

Azam FC imezifunga Simba SC na Yanga SC kabla ya kutwaa taji la Mapinduzi 2017 (Azam FC 4-0 Yanga SC mechi ya nusu fainali, Azam FC 1-0 Simba SC mchezo wa fainali)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad