Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepokea rufaa kutoka Klabu ya Polisi Dar es
Salaam dhidi ya Klabu ya Simba kuhusu kumchezesha Mchezaji Novalty Lufunga
katika mchezo wao wa Raundi ya Tano ya Kombe la Azam Sports Federation Cup
2017.
Madai ya
Polisi ni kwamba Mchezaji Novalty Lufunga alioneshwa kadi nyekundu kwenye Simba
dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Azam Sports Federation Cup 2015/2016
uliofanyika Uwanja wa Uhuru, Januari 22, mwaka huu.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetupilia mbali rufaa hiyo kwa kukosa vigezo
vya kikanuni katika uwasilishaji wake na hivyo kukosa sifa ya kusikilizwa. Hii
ni kwa mujibu wa kanuni ya 18 (1) na (2) ya Kanuni za Kombe la Shirikisho la
Azam Sports HD.
Kanuni ya 18
(1) inasema: “Malalamiko yoyote kuhusiana na mchezo yawasilishwe kwa maandishi
kwa kamishna wa mchezo au TFF sio zaidi ya masaa sabini na mbili (72hrs) baada
ya kumalizika mchezo.”
Kanuni ya 18
(2) inasema: Ada ya malalamiko ni shilingi laki tatu (Tshs 300,000.00).
Malalamiko yo yote yatakayowasilishwa bila kulipiwa ada na kuwasilishwa nje ya
muda uliowekwa hayatasikilizwa.”
Hata hivyo,
Shirikisho linapenda kutoa ufafanuzi kuhusu kadi nyekundu aliyopewa Mchezaji
Novalty Lufunga katika mashindano ya Azam Sports Federation Cup 2016/2017.
Kwa
utaratibu wa mashindano haya ambayo ni ya mtoano, adhabu za kadi (njano na
nyekundu) zitolewazo uwanjani, zinakoma mwisho wa msimu wa shindano husika
isipokuwa kadi hizo zikiongezwa adhabu ya kinidhamu (suspension) ambayo
itafahamisha kwa klabu na mchezaji kwa maandishi.
Kadhalika,
Kanuni ya 16 ya Kanuni za Kombe la Shirikisho Sehemu ya Tatu inaeleza wazi kuwa
matumizi ya kanuni za ligi zitahusika maeneo yanayoruhusu uendeshaji wa
shindano la mtoano.
“Adhabu zote
zinazohusisha katika mashindano ya Kombe la Shirikisho la Azam HD zitahusisha
na shindano hili tu,” inasema kanuni ya 16 (3) na (4).
..…………………………………………………………………………........................
IMETOLEWA NA
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
|
No comments:
Post a Comment