Akizungumza
kwa njia ya simu, Msemaji wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Midladjy Maez
alisema ajali hiyo ilitokea saa 9:40 alasiri katika Kitongoji cha Kambini Ruvu
Ngeta, Kata ya Kikongoa Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani. Maez alisema mabehewa
hayo yalianguka baada ya treni kuacha njia na kusababisha majeruhi kadhaa.
“Ni kweli
ajali hiyo imetokea na kusababisha majeruhi na hadi wakati huo kulikuwa hakuna
taarifa yoyote ya kifo kilichotokana na ajali hiyo, licha ya kwamba mtu mmoja
ndiyo hali yake mbaya,” alisema Maez, bila kutaja sababu za ajali hiyo.
|
“...Imeripotiwa
watu kadhaa wamejeruhiwa na mmoja amejeruhiwa sana, hizi ni taarifa za
awali…baada ya kikosi cha uokoaji kumaliza kazi ya kuinua mabehewa ndio taarifa
ya waathirika itakamilika,” alisema Maez katika taarifa yake.
Alisema
treni hiyo ilitakiwa ifike Dar es Salaam saa 11 jioni, lakini ilipofika hapo
mabehewa hayo yalianguka na kusababisha kushindwa kuendelea na safari.
“Kutokana na
ajili hiyo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa
na Mkurugenzi Mkuu wa TRL wanaelekea eneo la tukio ili kuweza kujua
kilichotokea,” aliongeza msemaji huyo wa TRL.
|
No comments:
Post a Comment