Mikoa 17 Tanzania yafadhiliwa Miradi ya maji na Serikali ya India. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, January 27, 2017

Mikoa 17 Tanzania yafadhiliwa Miradi ya maji na Serikali ya India.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameishukuru Serikali ya India kwa ufadhili wake wa miradi ya maji katika miji 17 nchi ambayo inalenga kupunguza tatizo la maji kwa wananchi wengi nchini.

    Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza katika ufunguzi huo.

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo Jijini Dar es Salaam katika hafla ya Maadhimisho ya miaka 68 ya Siku ya Kitaifa ya Jamhuri ya India sherehe ambazo zimeambatana na uzinduzi rasmi wa majengo ya ofisi mpya ya ubalozi wa India hapa nchini.

Makamu wa Rais pia ameishukuru Serikali ya India kwa msaada wake wa shilingi milioni 500 alioutoa kwa wananchi wa Mkoa wa Kagera ambao walikumbwa na tetemeko la ardhi mwaka jana(September 10,2016.

Mhe.Samia pia ametoa salamu za rambirambi kwa Serikali ya India kufuatia ajali ya treni iliyotokea katika Jimbo la Andhra Pradesh na kusababisha vifo vya watu 30 na kujeruhi wengine.
 Balozi wa India nchini Tanzania, Bw.Sandeep Arya.

Kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania napenda kutoka salamu za Pole kwa familia za wafiwa na majeruhi katika kipindi hiki kigumu kwa kumwomba Mwenyezi Mungu azipumzishe roho za marehemu mahali pema peponi na tunawaombea majeruhi wapone haraka. ’’

Kwa upande wake, Balozi wa India hapa nchini ,Bw.Sandeep Arya amemhakikishia Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Serikali ya India itaendelea kudumisha na kuendeleza mahusiano mazuri yaliyopo kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa pande zote Mbili.

Tazama hapa Chini  shughuli ilivyokuwa wakati wa Ufunguzi wa majengo mapya ya ubalozi wa India nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad