Ligi Mkoa wa Kagera: Bingwa Mtetezi Murusagamba FC yaifumua Kombora FC bao 11-1. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, January 20, 2017

Ligi Mkoa wa Kagera: Bingwa Mtetezi Murusagamba FC yaifumua Kombora FC bao 11-1.


Uwanja wa Kaitaba –Bukoba/Kagera.

Ligi Taifa daraja la 3 mkoani Kagera imeendelea leo,Ijumaa January 20,2017 kwa michezo miwili kuchezwa saa nane mchana na saa 10 jioni katika uwanja wa Kaitaba ambapo Kagera United kucheza na Halmashauri Misenyi huku Mabingwa watetezi Murusagamba FC ya Ngara kucheza na Kombora FC ya Muleba.
 Matokeo ya mchezo wa Kwanza –kwa mujibu wa Katibu mkuu wa chama cha Soka mkoani Kagera -KRFA- Salum Umande Chama- Kagera  United waeshinda mabao 3-0 dhidi ya Halmashauri Misenyi huku Murusagamba FC wakijiimarisha kuutetea Ubingwa wao kwa kucheza Mtu 9 tu kwa Kuwafunga Kombora FC mabao 11-1.

Mpaka sasa kundi A timu zilizofuzu kwenda hatua ya Robo fainali kutoka kituo hicho ni Majengo FC na Muleba Stars walkimaliza mechi zao za kundi huku Kundi B- Timu ya Kagera United ikitangulia kufuzu kwa kufikisha alama 10 huku akiwasubiri kati ya Murusagamba FC wenye alama 7 au Vatican City wenye alama 6 ambapo wataamuana nani aungane na Kagera United hapo january 22,mwaka huu watakapocheza mchezo wao wa mwisho wa Kundi hilo.

Timu hizo zitaanza hatua ya robo fainali  January 24,2017 kwa mshindi wa kwanza kundi A kucheza na mshindi wa pili kundi B huku robo fainali ya pili ikipigwa january 25 kwa mshindi wa kwanza kundi B kucheza na Mshindi wa kwanza kundi A.

Tayari Makamu Bingwa wa msimu uliopita ,Nzaza FC ya wilayani Ngara na Eleven Stars ya Misenyi zimefuzu kutoka kituo cha Karagwe na sasa wanawasubiri washindi wawili watakao fuzu kutoka kituo cha Bukoba ili kucheza Ligi itakayotoa Bingwa wa Mkoa wa Kagera wa Ligi hiyo kwa Msimu huu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad