HABARI/PICHA:Trump Aanza Kazi Marekani. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, January 21, 2017

HABARI/PICHA:Trump Aanza Kazi Marekani.

Bwana Donald Trump amechukua hatamu kutoka kwa Rais Barack Obama baada ya kuapishwa hapo Jana January 20,2017,saa mbili usiku kwa muda wa Afrika Mashariki. 

Wafuasi wake walikusanyika kwa wingi barabara za Washington.

Donald Trump anakuwa rais wa 45 wa Taifa la Marekani na amerejelea ahadi yake ya kampeni ya kuifanya nchi yake kuwa taifa lenye nguvu zaidi kuliko hapo awali, Hata hivyo maelfu waandamana nchini Marekani kupinga kuapishwa kwake.

Rais wa 45 wa Marekani, Donald Trump pamoja na familia yake wakifurahia mara baada ya kumaliza kuapishwa kwa rais mpya wa Marekani,ma hapa chini akihutubia taifa kwa mara ya kwanza mara baada ya kuapishwa kuwa rais wa Taifa hilo.

Rais wa Marekania (Pichani) Donald Trump ameanza kutia saini maagizo ya rais ,baadhi yake yakiwa ni ya kubadili yale yalioafikiwa na mtangulizi wake Barak Obama.

Muda mfupi baada ya kukagua gwaride la kuapishwa kwake, Bwana Trump, alitia amri ya serikali, kupunguza mzigo wa kiuchumi kwa taifa, unaotokana na gharama za kufadhili bima ya matibabu ya bei nafuu inayofahamika kama Obama Care, ambayo Trump aliahidi kufanyia marekebisho.

Trump pia ametia saini amri ya kuwaidhinisha mawaziri wake wapya wa Ulinzi na usalama wa kitaifa ambao uteuzi wao umepitishwa na bunge la seneti.

Utawala wa Trump pia umeaanza kufanyia marekebisho mtandao wa kijamii wa Ikulu ya White House kwa kuweka masuala yatakayopatiwa kipaumbele na uongozi huo mpya.

Rais wa 45 wa Marekani, Donald Trump(mwenye tai nyekundu) akimsindikiza rais aliyemaliza muda wake Barack Obama pamoja na aliyekuwa Makamu wa rais wake.

Baadhi ya wananchi waliokuwa wanashuhudia kuapishwa kwa Donald Trump.

Rais wa Marekani, Donald Trump akipeana mkono na rais aliyemaliza muda wake Barack Obama.
 
Rais aliyemaliza muda wake Barack Obama akiwapungia mkono.
Herikopta  iliyombeba rais aliyemaliza muda wake Barack Obama pamoja na mke wake ikiondoka.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad