Wanafunzi wa
shule ya msingi Nshanje kata ya Kyebitembe wilayani Muleba mkoani Kagera wakisomea
chini ya miembe kutokana wa changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa
ambapo Kamera yetu imepita na kujionea
hali halisi
Pia shule
hiyo haina nyumba hata moja ya walimu licha ya kuwa na walimu 9 na iliyojengwa
miaka 10 iliyopita, imeishia renta huku Serikali ya kijiji cha Kasindaga
ikijenga ya miti ili walimu hao wapunguze kutembea umbali wa kilomita 18 kila
siku kwenda kufundisha wanafunzi wa shule hiyo.
|
Walimu wa shule hiyo na wanafunzi pamoja na Mwenyekiti wa kijiji cha Kasindaga Mathias Bishobo wamethibitisha kuwepo wa changamoto hizo na kwamba Wananchi wanajitahidi kuchangia vifaa vinavyopatikana kwenye mazingira yao ili kuboresha miundombinu ya kufundishia na kujifunzia na kuiomba serikali kuchangia vifaa vya ujenzi vitokavyo viwandani
Habari na picha kwa hisani ya mwandishi wetu Shaaban Ndyamukama kutoka wilayani Muleba.
|
No comments:
Post a Comment