|
Mkuu wa
wilaya ya Buhigwe mkoa wa Kigoma kanali Marco Gaguti akifafanua jambo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya
Mabanda Mkoa wa Makamba nchini Burundi,(Musitanteri) Niyonkuru Laetitia, pamoja
na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Tanzania na Burundi katika kujadiliana sakata
la Wahamiaji wengi wengi kuanza kuingia nchini Tanzania kwa kasi tangu
Januari,2017.
|
Mkuu wa
wilaya ya Buhigwe mkoa wa Kigoma kanali Marco Gaguti akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Mabanda Mkoa wa Makamba
nchini Burundi,(Musitanteri) Niyonkuru Laetitia.
|
Mkuu wa
Wilaya ya Buhigwe akiongozana na kamati ya ulinzi na usalama kuingia mpakani
mwa Burundi na Tanzania.
Na Rhoda
Ezekiel Kigoma.
Mkuu wa
wilaya ya Buhigwe mkoa wa Kigoma kanali Marco Gaguti amewaonya wakimbizi wenye
historia ya uhalifu nchini Burundi
wanaoingia Nchini Tanzania, kwa
kigezo cha kuomba hifadhi ya ukimbizi kwa kuhofia wasikamatwe kwa uhalifu
walioufanya Nchini mwao, kuwa ikibainika
hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Aidha,
Gaguti aliuomba uongozi wa Nchi ya Burundi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya
ulinzi na usalama vya Wilaya hiyo
iliyopo Mpakani, kuwabaini waomba hifadhi
hao wanaoingia Nchini kwa kukimbia uhalifu walioufanya Nchini mwao na
kuja kuendeleza vitendo hivyo wanapo ingia Nchini.
Hayo
yalibainika jana wakati wa Kikao cha majadiliano baina ya Mkuu huyo na Mkuu wa
Wilaya ya Mabanda Mkoa wa Makamba Nchini Burundi, alipokuwa akihoji ni kwanini wahamiaji
wengi wanaongezeka Nchini wakidai wanakimbia vurugu zinazo endelea Nchini mwao
ambapo kwa Mwezi january waliingia
waomba hifadhi 2230, ambapo ilibainika wengi wao wanadai wanakimbia kukamatwa
kwa kujihusisha na uhalifu na wengine kukimbia njaa iliyopo majumbani kwao.
Gaguti
alisema kumekuwa na ongezeko kubwa la wahamiaji wanaoingia Nchini wakidai
kukimbia vitisho wanavyo pewa na kikundi cha Vijana wa chama tawala kinacho
julikana kama ( IMBONELAKULE), ambapo wanakuja kuomba hifadhi katika Nchi ya
Tanzania ilihali Nchi yao ina amani ya kutosha
na wengine kukimbilia kambini kupata huduma za bure kwa kuhofia njaa
nchini mwao .
Hali
iliyopelekea Waziri wa Mambo ya ndani kusitisha zoezi la Waomba hifadhi kuingia
Nchini kwa kigezo cha kukimbia njaa Nchini mwao na kukimbilia Tanzania ili
waweze kupata Msaada wa chakula , ni lazima Afanyiwe mahojiano na atoe sababu
zilizo mfanya akimbie iliaweze kupatiwa kibali cha kuwa mkimbizi.
Hata hivyo
Kanali Gaguti aliwaomba viongozi hao kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na
usalama kuwabaini wahalifu hao waweze kurudishwa Nchini mwao kuepukana na
vitendo vinavyo endelea na ongezeko la waomba hifadhi kuingia Nchini bila
kufuata utaratibu.
'' leo
nilikuwa natembelea vituo na kuona ongezeko la wahamiaji lakini serikali imetoa
maelekezo mapya ikiwemo kuwatambua na kujua sababu za kukimbia Nchini mwao,
lakini kama atakuwa na sababu za Msingi hata pata fursa ya kuwa mkimbizi,
lakini pia nikuombe ushirikiano kama kuna taarifa za watu ambao ni wahalifu
upewe taarifa mapema kabla ya mambo kubadilika ili tuweze kuchukua tahadhari
mapema kwa pande zote mbili" alisema kanali Gaguti.
Naye mkuu wa
Wilaya ya Mabanda Mkoa wa Makamba (Musitanteri)Niyonkuru Laetitia alisema kwa
sasa nchi ya Burundi ni tulivu na wanaokimbia nchini mwao ni wale wanaokimbia njaa na wengine
kukimbia uhalifu aliofanya nchini Burundi na kuja Tanzania kuomba hifadhi.
Alisema
wengi waliofika Tanzania ni wale waliokimbia kwa mambo yao binafsi na wengine
ni wale wakimbizi waliorudishwa Burundi kipindi cha nyuma wanaokimbia wengi
wanakuja kwa kigezo cha kupelekwa nje ya Nchi kama vile America na Ulayana Nchi
nyingine ilikuwafuata ndugu zao walio pelekwa huko .
Aidha
aliuomba Uongozi wa Tanzania kabla ya kuwapokea wahamiahi hao kuchukua
vitambulisho vyao ilikubaini walio kimbia tuhuma zinazo wakabili, pia kumekuwa
na tetesi wengi wao wanaoingia kuomba hifadhi wanakuja makambini kujifunza
namna wanavyo weza kwenda kuipindua Nchi kwa kupigana pindi wanapo wabaini
waweze kuwakabidhi kwa Serikali ya Burundi.
Kwa upande
wao baadhi ya Waomba hifadhi waliofika katika maeneo ya kupokelea waomba
hifadhi hao kwa mahojiano waweze kuingia kambini ,wengi wao walidai wanakimbia
vikundi vya IMBONELAKULE vinavyo wafuata Nyumbani kwao usiku na kuwapiga na
kuwatishia usalama wao hali inayo walazimu kukimbilia Tanzania , suala lililo
kanushwa na Mkuu wa Wilaya ya Mabanda.
Nizigimana
Silivesta ni moja kati ya waomba hifadhi
kutoka Burundi, alisema kinacho wapelekea kukimbia Nchini mwao ni hali ya
kiusalama kuwa ndogo kumekuwa na tabia ya vikundi vya watu vinavyo wafuata
kuwatisha kutokana na baadhi ya ndugu zao walio kimbilia nchini kuwa
wanamahusiano nao na wanaipinga serikali.
|
No comments:
Post a Comment