Morocco Pichani
imewavua ubingwa Ivory Coast baada ya kuwafunga goli 1-0 na kwenye mchezo wa
mwisho wa Kundi C kisha Morocco kufuzu kucheza robo fainali ya michuano hiyo
mikubwa ya soka la Afrika kwa timu za taifa.
Shuti la
Rachid Alioui akiwa umbali wa mita 25 liliipa Morocco ushindi pamoja na kocha
wao Herve Renard, ambaye aliiongoza Ivory Coast kutwaa ubingwa wa Afrika mwaka
2015.
|
Mechi za
mwisho za Kundi D la AFCON 2017, Mashindano ya 31 ya Fainali za Kombe la
Mataifa ya Afrika, zimekamilika Jana January 25,2017 usiku Nchini Gabon na
kukamilisha safu ya Mechi za Robo Fainali baada ya Egypt kuilaza Ghana 1-0 na
kufuzu na kuungana na hao Ghana waliofuzu kabla ya mechi hiyo.
Bao la
ushindi ambalo limeiingiza Egypt robo Fainali limefungwa Dakika ya 11 na
Mohamed Salah.
Katika Mechi
nyingine ya Kundi D, Uganda walitangulia kufunga Dakika ya 70 kwa Bao la Farouk
Miya na Mali kurudisha Dakika ya 73 kwa Frikiki ya Yves Bissouma.
Robo Fainali
zitaanza kuchezwa Jumamosi January 28,2017.
Ratiba/Matokeo:Robo
Fainali
Jumamosi
Januari 28,2017.
1900 Burkina
Faso v Tunisia
2200 Senegal
v Cameroon
Jumapili
Januari 29,2017.
1900 Congo
DR v Ghana
2200 Egypt v
Morocco
Nusu Fainali
Jumatano
Februari 1,2017.
2200 Mshindi
RF 1 v Mshindi RF 4
Alhamisi
Februari 2,2017.
2200 Mshindi
RF 2 v Mshindi RF 3
Mshindi wa 3
Jumamosi
Februari 4,2017.
2200
Aliefungwa NF 1 v Aliefungwa NF 2
Fainali
Jumapili
Februari 5,2017.
2200
Finalist 1 v Finalist 2
NCHI
ZILIZOWAHI KUTWAA UBINGWA WA AFRIKA.
-Egypt-Mara
7
-Cameroon,
Ghana-Mara 4
-Nigeria-Mara
3
-Congo
DR-Mara 2
-Zambia,
Algeria, Congo, Ethiopia, Ivory Coast, Morocco, South Africa, Sudan,
Tunisia-Mara 1
|
No comments:
Post a Comment