Diego Costa na Henrikh Mkhitaryan wazipa Ushindi Chelsea na Manchester United. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, December 11, 2016

Diego Costa na Henrikh Mkhitaryan wazipa Ushindi Chelsea na Manchester United.

Chelsea wamerejea tena kileleni mwa Ligi kuu soka Nchini Uingereza 2016/2017- Premier League ni baada ya kushinda mchezo wao wa tisa mfululizo kufatia Diego Costa kufunga bao pekee la ushindi Dakika ya 76 walipoifunga West Bromwich Albion 1- 0  wakiwa uwanja wa nyumbani wa  Stamford Bridge mapema Leo December 11,2016.

Ushindi huu umewaweka tena Chelsea kileleni kwa kuwashusha Arsenal na wao sasa kuongoza EPL wakiwa na Pointi 37 wakifuata Arsenal wenye 34.
Mchezo mwingine wa leo kati ya Manchester United dhidi ya Tottenham Hotspur  na BAO la kwanza kwa Mchezaji Bora wa Bundesliga ya huko Ujerumani  Msimu uliopita 2015/2016,Henrikh Mkhitaryan dakika ya 29 limewapa Manchester United ushindi wa 1-0 dhidi ya Tottenham Hotspur Uwanjani Old Trafford.

Ushindi huu wa Manchester United umeikita Nafasi ya 6 wakiwa Pointi 3 nyuma ya Timu ya 5 Tottenham Spurs na 6 nyuma ya Timu ya 4 Manchester City.

Matokeo mengine ya gemu za leo tazama juu na hapa chini nimekuwekea  msimamo wa Ligi ulivyo baada ya mechi za leo December 11,2016..


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad