Rais Magufuli kuwania Tuzo la Mtu Mashuhuri. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, October 26, 2016

Rais Magufuli kuwania Tuzo la Mtu Mashuhuri.


Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ( pichani) ameteuliwa kuwania tuzo la Forbes la mtu mashuhuri wa mwaka.

Jarida hilo la biashara limemtambua Rais Magufuli kwa umuhimu wake katika kuimarisha uchumi wa taifa hilo.

 Wengine walioteuliwa kuwania tuzo hiyo ni pamoja na Benki ya Capitec nchini Afrika Kusini,Rais wa Mauritania,Mtetezi wa haki za umma nchini Afrika Kusini na Raia wa Rwanda.



Kama Rais Magufuli atafanikiwa kushinda tuzo hiyo, basi Tanzania itakuwa imepata tuzo hiyo kwa mara ya pili mfululizo kwani mwaka jana 2015, mshindi wa tuzo hiyo alikuwa Mkurugenzi Mtendaji na Rais wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji.

Utaratibu wa jinsi ya kupiga kura kwa mwaka huu ni kutumia tovuti ya FORBES AFRICA ambapo baada ya kuingia hapo, unaweza kugusa jina la mtu ambaye unapendekeza ashinde tuzo na hapo kura itakuwa imehesabiwa.



Na:BBC Swahili.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad