Madaktari Bingwa Wasaidia watoto wenye Vichwa vikubwa mkoani Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, October 25, 2016

Madaktari Bingwa Wasaidia watoto wenye Vichwa vikubwa mkoani Kagera.

mkuu-wa-mkoa-wa-kagera-meja-jenerali-mstaafu-salum-kijuu-akiwashukuru-wawakilishi-wa-kambi-tiba-ya-gsm-foundation-ofisini-kwake-copy-copy
Mkuu wa mkoa wa Kagera meja jenerali  mstaafu Salum Kijuu akiwashukuru wawakilishi wa kambi tiba ya GSM Foundation ofisini kwake,Dk Hamis alisema kuwa utafiti uliofanywa na Taasisi ya MOI mwaka 2002 unaonyesha zaidi ya watoto 4800 huzaliwa kila mwaka wakiwa na maradhi ya vichwa vikubwa na migongo wazi na kati yao 500 pekee ndiyo wanaoweza kufika hospital na kupatiwa matibabu.

Akizungumzia chimbuko la maradhi hayo Dk Hamisi alisema kuwa watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi wanaweza kuzaliwa nacho au kupata siku chache baada ya kuzaliwa.
one
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu(kulia) akiwaameongozana na kaimu mkuu wa kambi tiba za GSM Foundation Dk Hamis Shaaban wodini kuangalia watoto.Kulia ni mzazi Joviti Mchuruza

Kwa wale wanao zaliwa na maradhi hayo ni kwasababu ya upungufu wa virutubisho ambavyo mama mjamzito anatakiwa avipate kabla ya kushika mimba virutubisho hivo vinapatikana kwenye matunda,mboga za majani,mayai na vyakula vyote vyenye protini, pia maradhi ya mgongo wazi husababisha watoto kupooza na kushindwa kutumia miguu yao,” >>> DK Hamis

Alisema mpaka sasa kwa Mkoa wa Kagera wameshawafanyia upasuaji jumla ya watoto saba wenye vichwa vikubwa na mmoja wa mgongo wazi.Ofisa habari wa GSM Foundation Khalfani Kiwamba alisema kuwa taasisi yao iliamua kudhamini matibabu ya maradhi ya vichwa vikubwa na migongo wazi baada ya kuelezwa changamoto mbalimbali za matibabu ya maradhi hayo na uongozi wa Taasisi ya MOI.

picha-ya-pamojaya-wana-kambi-tiba-baada-ya-kumaliza-kazi-kagera-copy
Picha ya pamoja ya wana kambi tiba baada ya kumaliza kazi Kagera

Joviti Mchuruza akiongea kwa niaba ya wazazi ambao watoto wao wamefanyiwa upasuaji aliwashukuru timu nzima ya madaktari hao pamoja na Taasisi ya GSM kwa msaada huo wa matibabu waliowapatia wa watoto wao bure. Aliiomba jamii kuacha kuhusisha maradhi hayo na mila potofu za imani za kishirikina au mikosi kwenye familia hali inayofanya akina mama au baba kutelekezewa watoto.

Aliwaomba pia wataalam hao wasogeze huduma hiyo karibu na jamii hasa maeneo ya vijijini ambapo wapo watoto wengi wenye maradhi hayo wanateseka na hawana msaada.

Nawaomba wazazi wenzangu hasa akinamama sababu sisi ndiyo tunakaa na watoto kwa muda mrefu ndiyo tunaoweza kugundua mabadiliko ya mtoto pia tusisikilize maneno ya dhihaka ya watu wa pembeni maradha haya yanatibika kabisa”>>> Joviti Mchuruza

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu aliwashukuru madaktari pamoja na shirika la GSM Foundation kwa udhamini huo wa matibabu bure kwa watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi.

Pia aliwataka wazazi wenye watoto wenye maradhi hayo wasione aibu kuwapeleka hospitali ili waweze kupatiwa matibabu bure.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad