Mkuu wa
Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari
(hawapo pichani),mapema leo wakati alipokuwa akipokea msaada wa vitanda na
magodoro 18 kutoka katika kampuni ya taasisi za kifedha NMB Kanda ya magharibi
Tabora tawi la Kakonko, lengo likiwa ni kuchangia kupunguza vifo vya mama na
Mtoto katika wilaya ya Kakonko Mkoani wa Kigoma.
Na Rhoda Ezekiel -Globu ya Jamii
Kigoma.
Mkuu wa
Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala ameipongeza idara ya Afya Wilayani
Kakonko kwa jitihada ya kupungua kwa vifo vya mama na mtoto kutoka vifo 404
Kati ya vizazi hai 100,000 kwa mwaka kutokana na wadau wa Afya kuchangia Huduma
hiyo kww ushiriki wa pamoja na watumishi wa idara ya afya.
Kauli hiyo
imetolewa wakati mkuu huyo akipokea msaada wa vitanda Na magodoro 18 kutoka
katika kampuni ya taasisi za kifedha NMB Kanda ya magraribi Tabora tawi la
Kakonko lengo likiwa ni kuchangia kupunguza vifo vya mama Na Mtoto katika
wilaya ya Kakonko Mkoa wa Kigoma.
Ndagala
alisema jitihada zinazofanywa na wadau pamoja na idara ya afya zinaonyesha wazi
kuwa vifo hivyo vitazidi kupunguza siku hadi siku.Licha ya kuwepo jitiada za
kufikia malengo hayo sekta ya afya bado inakabiliwa matatizo mbalimbali ikiwa
ni pamoja na madawa vifaa tiba na miundo mbinu hatua inayoilazimu serikali
Taasisi na wadau mbambali kujitoa kwa ajili ya kuboresha huduma za afya.
Aidha Mkuu
huyo wa Wilaya aliipongeza Benk hiyo kwa msaada ulioutoa katika hospital ya
wilaya na kuwaomba watumishi na wananchi kuvilinda vitanda Na magodoro
yaliyotolewa ilikuwezakusaidia Wananchi Na Serikali kwa ujumla ilikuweza
kupunguza kabisa ya ukosefu wa vitanda.
Nae Meneja
wa benki ya NMB tawi la Kakonko,Bw.Leonard Mgaya alisema benk hiyo imeamua
kuboresha mazingira ya kujifugulia kwa wanawake ilikupunguza vifovitokanavyo na
Huduma mbovu zinazotolewa katika vituo vya Afya Benki hiyo imetoa msahada wa
Vitanda na Magodoro 18 yenye thaman ya tsh milion kumi katika kituo cha Afya
Kakonko kinachotumika kama hospitali ya wilaya ambapo msahada wa awamu ya
kwanza vitanda 9 ulitolewa mwezi tisa .
Kwa upande
wake Mganga mkuu wa wilaya ya kakonko Joseph Tutuba amesema katika wilaya yake
vifo vya wanawake wajawazito vimepungua kwa chini ya wastani ya vifo 404 kati
ya 100,000 hali ambayo ni chini ya zaidi wastani wa kitaifa ambao ni 432 kwa
vizazi hai na kudai kuwa hatu hiyo ni kutokana na kutumia ipasavyo michango
inayotolewa na wadau wa afya.
|
No comments:
Post a Comment