NIDA na Zoezi la Utoaji Vitambulisho Vya Taifa vyenye Saini September 14,2016. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, September 12, 2016

NIDA na Zoezi la Utoaji Vitambulisho Vya Taifa vyenye Saini September 14,2016.

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) itaanza kutoa Vitambulisho vipya vya Taifa vyenye saini kwa wananchi wote waliokamilisha taratibu za usajili na utambuzi na kuchukuliwa alama za kibaiolojia (Alama za vidole, Picha, Saini ya Kielektroniki).

Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Bw. Andrew Massawe; utekelezaji wa zoezi hilo utaanza rasmi Jumanne tarehe 14 Septemba 2016 , katika ofisi zote za NIDA zikiwemo ofisi za Wilaya zilizoanza usajili Tanzania ,Zanzibar na mikoa ya Dar-es-salaam, Pwani, Lindi, Mtwara, Morogoro, Tanga, Arusha, Kilimanjaro, na Ruvuma) pamoja na waheshimiwa Wabunge Dodoma.

Kwa sasa vitambulisho vya Taifa vimeanza kutumika katika baadhi ya huduma nchini hususani kwenye mabenki kwa ajili ya kufungua akaunti na kuthibitisha taarifa za mtu kabla ya kupatiwa huduma.  Taratibu za kupanua wigo wa matumizi ya Vitambulisho kielektroniki kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali zinaendelea.

Waombaji wote ambao Vitambulisho vyao viko tayari watatumiwa ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) katika simu zao za kiganjani (mkononi) kufahamishwa kufika katika vituo vya Usajili kuchukua Vitambulisho vyao.

Kuhusu wananchi ambao tayari wana Vitambulisho visivyo na saini; Bw. Massawe amesema…. “ Mamlaka inakusudia kubadilisha vitambulisho vyote vya zamani visivyo na saini, ila kwa sasa vitambulisho vya zamani vitaendelea kutumika sambamba na vipya wakati taratibu za kuendelea kuvibadilisha zikiendelea” alisisitiza.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad