Ligi kuu Vodacom 2016/2017-Simba yajitanua Taifa, yaua 4-0. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, September 24, 2016

Ligi kuu Vodacom 2016/2017-Simba yajitanua Taifa, yaua 4-0.

Timu ya Simba SC imezidi kutanua kwapa kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2016/2017 baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Maji Maji ya Songea jioni ya leo Septemba 24,2016 katika mchezo huo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ushindi huo uliotokana na mabao ya Jamal Simba Mnyate mawili na moja la Shizza Ramadhani Kichuya, unaifanya Simba SC ifikishe pointi 16, baada ya kucheza mechi sita, wakishinda tano na sare moja. 

Simba ikapata pigo dakika ya 21 baada ya mshambuliaji wake tegemeo, Ibrahm Hajib kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo, nafasi yake ikichukuliwa na kiungo Said Ndemla.
Shizza Ramadhani Kichuya akaifungia Simba SC bao la pili kwa penalti dakika ya 67 baada ya beki wa Maji Maji, Lulanga Mapunda kuunawa mpira kwenye boksi.

Mnyate akawainua tena wapenzi wa SImba vitini kwa kufunga bao la tatu dakika ya 74 akimalizia krosi ya Mo Ibrahim

Kichuya akakamilisha sherehe za mabao za Simba SC kwa kufunga la nne dakika ya 81 baada ya kumlamba chenga kipa mkongwe wa Maji maji, Amani Simba baada ya pasi ndefu ya Nahodha Jonas Gerald Mkude. 
Baada ya ushindi huo, Simba SC inakwenda kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya mahasimu wao, Yanga SC Jumamosi wiki ijayo ,Octoba Mosi,2016 kwenye Uwanja huo huo wa Taifa.  

Ligi Kuu inaendelea kesho,Jumapili Septemba 25,2016  kwa mechi mbili; Ruvu Shooting na Toto Africans Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani, Stand United na Yanga SC Uwanja wa Kambarage, Shinyanga na kesho African Lyon itamenyana na Kagera Sugar Uwanja wa Taifa.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad