Ndanda FC Waiangusha i Azam FC kwa mabao 2-1. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, September 24, 2016

Ndanda FC Waiangusha i Azam FC kwa mabao 2-1.

Timu ya NDANDA FC imewaangusha washindi wa Ngao ya Jamii AZAM FC kwa mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Nangwanda SIjaona, Mtwara leo,Jumamosi Septemba 24,2016.

Mabao ya Ndanda yamefungwa na Riffat Khamis na Hajji Mponda, wakati la Azam FC lilifungwa na Nahodha John Raphael Bocco.

Hicho kinakuwa kipigo cha pili mfululizo kwa Azam FC baada ya wiki iliyopita kufungwa 1-0 na Simba SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Matokeo hayo yanaifanya Azam FC ibakie na pointi zake 10 baada ya kucheza mechi sita, wakifungwa mbili, sare moja na kushinda tatu.
Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, JKT Ruvu wameshinda 2-0 dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani, Prisons wametoka sare ya 0-0 na Mwadui FC Uwanja wa Sokoine, Mbeya na Mtibwa Sugar imelazimishwa sare ya 1-1 na Mbao FC Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad