Shirika la Marafiki wa Afrika na Kituo cha Elimu ya Afya kwa Jamii wilayani Ngara mkoani Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, August 21, 2016

Shirika la Marafiki wa Afrika na Kituo cha Elimu ya Afya kwa Jamii wilayani Ngara mkoani Kagera.


Shirika la Marafiki wa Afrika kwa kushirikiana na wafadhili kutoka nchini Ujerumani limetoa Sh Milioni 10 kwa ajili ya kujenga kituo cha Elimu ya Afya kwa jamii katika shule ya Sekondari ya Wasichana Baramba wilayani Ngara mkoani Kagera kuwasaidia wakazi wa jirani na shule hiyo kupima maradhi mbalimbali kabla ya kwenda Hospitali.


Mwenyekiti wa Shirika la Marafiki wa Afrika Tanzania, Bw Isayas Bambara ambaye ni Meneja wa Shule hiyo ,ametoa taarifa hiyo jana kwenye uzinduzi wa kituo hicho ambacho watu watapima magonjwa na kupata elimu ya kujikinga na visababishi vya maradhi kwenye maeneo yao.

Amesema lengo la kituo hicho ni kupunguza vifo vya wanawake na watoto chini ya miaka mitano wanaopata tabu kwa kutembea umbali mrefu kutafuta huduma katika kituo cha afya Lukole au hospitali ya Nyamiaga na kusababisha wasiojiweza kifedha kufariki.

Mgeni rasmi katika uzinduzi wa kituo hicho, Mbunge wa jimbo la Ngara Bw Alex Gashaza amechangia Sh1.2 milioni, kwa ajili ya upanuzi wa vyumba vya kutolea huduma. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad