Waziri Ummy Mwalimu Pamoja na Wenyeji Wake Wakiongozwa Mhe.
Kijuu Mkuu wa Mkoa Wakitembelea Nyumba za Watumishi wa Makazi ya Wazee Kiilima-Bukoba.
Aidha, Waziri Ummy aliwaagiza Maafisa Ustawi wa Jamii
kuwatembelea wazee hao mara kwa mara ili kuwapatia msaada wa kisaikolojia na
kutambua Wazee ambao bado wanao ndugu na jamaa waweze kusaidiwa ili kurudishwa
kwa ndugu na jamaa zao.
Pia Waziri Ummy
Mwalimu alisema kuwa kwasasa Wizara yake imeamua kubadilisha jina badala ya
kuendelaea kuitwa Vituo vya kuwatunza Wazee
sasa yanaitwa Makazi ya wazee, jina la “vituo” ilionekana kuwa ni kama kuwanyanyapaa
wazee hao.
Changamoto zinazoyakabili makazi ya wazee Kiilima ni ubovu wa
miundombinu kama vyoo, bweni moja ndilo linalotumika la wanawake badala ya
mabweni mawili, majengo yote yamechoka yanahitaji urabati pia kuna tatizo la
uhaba wa chakula, huduma za afya na usafiri wa kuwasafirsha Wazee kwenda kwenye
matibabu, aidha, watumishi wa kituo hicho hawatoshi.
Makazi ya Wazee Kiilima yanawatunza Wazee 18 Wanawake 4 na Wanaume
14.
Wazee hao walimshukuru Mhe. Waziri Ummy kwa kuwatembelea na kujionea changamoto
walizo nazo katika makazi yao, pia walimshukuru mlezi wao Bi Gladness Rwiza kwa
kujitoa kwa hali zote katika kuwahudumia hasa katika upande wa chakula.
|
No comments:
Post a Comment