SHERIA/KANUNI/TARATIBU:-Wauza Dawa na Vipodozi Mitandaoni Kukiona -TFDA. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, July 06, 2016

SHERIA/KANUNI/TARATIBU:-Wauza Dawa na Vipodozi Mitandaoni Kukiona -TFDA.

Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Umma kutoka TFDA, Gaudensia Simwanza.

Serikali kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imesema hivi karibuni itaanza msako mkali wa kuwatafuta na kuwakamata wauzaji wa dawa zinazokatazwa pamoja na vipodozi vikali ambao wanajitangaza kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii.

  Katika mahojiano na wanahabari, Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Umma kutoka TFDA, Gaudensia Simwanza alitaja bidhaa hizo kuwa ni dawa za kuongeza ukubwa wa viungo vya mwili, kupunguza uzito wa mwili na vipodozi vyenye kemikali za kuchubua ngozi bidhaa ambazo zinasababisha madhara makubwa kwa binadamu ikiwemo ugonjwa wa Saratani.

 “Kumezuka wafanyabiashara holela wanaotumia mitandao ya kijamii kama vile Instagram, Facebook, Whatsup Groups na kwengineko  kutangaza biashara ya dawa na vipodozi vyenye kemikali hatari ambavyo vimepigwa marufuku na TFDA hivyo wanaohusika wajiandae, hivi karibuni tutaanza kuwashughulikia.” Alisema Simwanza.

 Alieleza kuwa TFDA kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wameandaa mkakati madhubuti wa kuhakikisha wanawabaini na kuwakamata wafanyabiashara wote wanaouza dawa na vipodozi hivyo kupitia mitandao na kuwachukulia hatua ikiwemo kuwafikisha mahakamani au kuwatoza faini.

 Hivi karibuni kumeibuka wimbi la wafanyabiashara wa dawa mbalimbali pamoja na vipodozi ambao wanajitangaza kupitia mitandao ya kijamii na kuna baadhi ya watu wananunua bidhaa hizo bila ya kuhakikisha usalama wake jambo ambalo ni hatari kwa afya zao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad