TASWIRA PICHA:-Akutwa akiwa amefariki ndani ya Choo nje ya Nyumba yake wilayani Ngara.. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, July 05, 2016

TASWIRA PICHA:-Akutwa akiwa amefariki ndani ya Choo nje ya Nyumba yake wilayani Ngara..

Mwanamke Mercy Peter mwenye umri wa miaka 49 mkazi wa Kitongoji cha Mkachekeli mjini Ngara Mkoani Kagera amekutwa akiwa amefariki ndani ya choo nje ya nyumba yake.

Mwenyekiti wa Kitongoji hicho Bw Ernest Muhire amesema aliyegundua tukio hilo ni mtoto wa mwanamke huyo alipokwenda chooni kujisaidia leo, July 5, 2016 majira ya saa Mbili Asubuhi.


Amesema baada ya kugundua tukio hilo, mtoto huyo ametoa taarifa kwa uongozi wa Kitongoji ili kuwataarifu Polisi.

Jeshi la Polisi limethibitisha tukio hilo na kuruhusu mwili wa marehemu kuzikwa wakati uchunguzi ukiendelea.
Hata hivyo mmoja wa wataalamu wa Afya, Carist Karongo amesema kuwa hawajabaini chanzo halisi cha kifo hicho lakini hata hivyo baadhi ya majirani wanadai kuwa huenda ikawa ni njaa kwa kuwa mwanamke huyo alitoka kulewa usiku na kushindwa kula hivyo kuishiwa nguvu na kuanguka alipokwenda chooni.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad