PASHA MOTO SOKANI:-Jose Mourinho haamini macho yake baada ya kipigo kutoka kwa Borussia Dortmund. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, July 22, 2016

PASHA MOTO SOKANI:-Jose Mourinho haamini macho yake baada ya kipigo kutoka kwa Borussia Dortmund.

Kocha Jose Mourinho leo Julai 22,2016 ameonja joto la ugumu wa kuifundisha Manchester United baada ya klabu yake kupokea kipigo cha mbwa mwizi kutoka kwa Borussia Dortmund

Katika mchezo huo wa kirafiki uliopigwa Shanghai, China na kushuhudiwa na mashabiki 57,000, Manchester United ikachapwa 4-1 kama imesimama.

 Huu ni mchezo wa pili kwa Kocha Mourinho tangu arithi mikoba ya Louis van Gaal ambapo mchezo wa kwanza United ilishinda 2-0 dhidi ya Wigan.


Castro wa Borussia Dortmund akishangilia bao la kwanza sambamba na Ousmane Dembele na Shinji Kagawa.

Dortmund walitangulia kufunga Bao Dakika ya 19 kwa frikiki ya Aubameyang iliyomshinda Kipa Sam Johnstone na Aubameyang tena akafunga tena Bao kwa Penati katika Dakika ya 36.

Bao la 3 la Dortmund lilifungwa na Dembele Dakika ya 57 na Dakika 2 baadae Mchezaji wa zamani wa Dortmund Mkhitaryan akaipa Man United Bao lao moja.

Jose Mourinho kama haamini macho yake.

Dakika ya 65,  Dortmund walibadili Wachezaji 7 na Man United kubadili Wawili kwa kuwaingiza Paddy McNair na Januzaj badala ya Mkhitaryan na Blind.

Dakika ya 86 Dortmund, kuputia Castro wakafunga Bao lao la 4.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad