Na
Selemani Semunyu - JWTZ.
Klabu ya Golf ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya
Lugalo Jijini Dar es Salaam imeahidi kuendeleza Uwanja na klabu
hiyo na kuwa na mafanikio makubwa kimataifa ukilinganisha na klabu zingine za
Golf na kuwa kitovu cha Michezo na Uchumi kutokana na uwekezaji
katika Uwanja huo.
Hayo yamesemwa leo,Julai 03,2016 na Mwenyekiti Mpya wa klabu hiyo Brigedia
Jenerali Michael Luwongo wakati akikagua Uwanja wa Klabu hiyo ikiwa ni
mara ya Kwanza tangu kuteuliwa na kushika nafasi hiyo Jijini Dar es Salaam.
“Uwanja wa Klabu ya Golf ya Lugalo ndio uwanja wa Kwanza uliojengwa na
Wazalendo hivyo tunataka kuhakikisha unakuwa na hadhi ya kimataifa na kuzalisha
wachezaji watakaoletea taifa Ushindi” AlIsema Brigedia Jenerali Luwongo.
Brigedia Jenerali Luwongo alisema uwekezaji wenye lengo la kuwa kitovu
cha Michezo yote kwa kuwa viwanja bora licha ya kuendeleza michezo lakini
inaweza kuwa kitovu cha kiuchumi kutokana na wageni na wazawa kutumia viwanja
hivyo vitakavyokuwa na ubora wa Kimataifa.
Mwenyekiti huyo alisema mbali na Uboreshaji Miundombinu kazi kubwa
iliyoko mbele yake ni kuhakikisha Mchezo wa golf unachezwa na watu wa rika zote
lakini hasa vijana na Watoto ambao watakuwa tegemeo na hazina kubwa kwa Taifa.
Alisema kumekuwa na dhana isiyosahihi kuwa mchezo wa golf ni kwa matajiri
dhana ambayo ameipinga na kutaka watu wajitokeze katika Uwanja huo unaomilikiwa
na JWTZ ambao gharama za uchezaji wake ni ndogo ukilinganisha na klabu zingine.
“Uwanja ni wa Jeshi lakini sio kwamba Wanajeshi pekee ndio wa naruhusiwa
kuja kucheza hata ukiangalia wanajeshi wanaotumia uwanja huo ni ndogo
ukilinganisha na raia na wageni toka nje ya Nchi” Alisema Mwenyekiti.
Aidha alitoa Wito kwa Maofisa na Askari wa JWTZ kujitokeza kuwa wanachama
katika Klabu hiyo lakjini pia kushiriki mchezo wa Golf.
Kwa upande wake Msimamizi wa Miundombinu wa Klabu hiyo Kanali Mstaafu
Jackson Nsigaye amesema sasa wana viwanja 18 ambavyo ndio sahihi vya
Golf toka Viwanja Tisa walivyokuwa navyo awali na muelekeo ni kuwa na Viwanja
vya michezo mingine pia ili kiwe kituo cha michezo.
Naye Meneja wa Uwanja huo Kanali Omary alisema mpaka sasa ndio uwanja
pekee wenye mashindano mengi kuliko vilabu vyote na wataendeleza mafanikio hayo
katika mwaka huu.
Brigedia Jenerali Luwongo ameteuliwa kushika wadhifa huo na
Mlezi wa Klabu hiyo ambaye ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis
Mwamunyange kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Marehemu Brigedia Jenerali
Mstaafu Ernest Galinoma. |
No comments:
Post a Comment