KUFUZU FAINALI ZA U 17 AFRICA:-Serengeti Boys Yasonga mbele kwa Ushindi wa Jumla wa bao 9-0. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, July 03, 2016

KUFUZU FAINALI ZA U 17 AFRICA:-Serengeti Boys Yasonga mbele kwa Ushindi wa Jumla wa bao 9-0.

Timu ya taifa ya vijana ya Tanzaia chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imeshinda mabao 6-0 dhidi ya Shelisheli katika mchezo wa marudiano Raundi ya Kwanza kufuzu Fainali za U17 Afrika mwakani Madagascar jioni ya leo,July 3, 2016 Uwanja wa Stade Linite mjini Victoria. 

Kwa matokeo hayo, Serengeti Boys inasonga mbele Raundi ya Pili na hatua ya mwisho ya mchujo kwa ushindi wa jumla wa 9-0 baada ya wiki iliyopita kushinda 3-0 katika wa kwanza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Serengeti Boys
sasa itamenyana na Afrika Kusini, hayo yakiwa ni marudio ya mchezo wa mwaka jana katika hatua hiyo hiyo, ambayo vijana wa Tanzania walitolewa.

Mabao ya Serengeti Boys leo yamefungwa na Shaaban Zubeiry dakika ya sana, Mohammed Abdalah dakika ya 49, Hassan Juma mawili dakika ya 47 na 75, Issa Makamba kwa penalti dakika ya 65 na Yohana Nkomola dakika ya 90.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad