RATIBA / MATOKEO EURO 2016:-Mechi ya Ujerumani na Italia yaweka Rekodi hii Kubwa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, July 03, 2016

RATIBA / MATOKEO EURO 2016:-Mechi ya Ujerumani na Italia yaweka Rekodi hii Kubwa.

Mabingwa wa Dunia Ujerumani wameondoa gundu kwa kuitungua Italia kwa Penati 6-5 kufuatia Sare ya 1-1 katika Dakika 120 za Mchezo wa Robo Fainali ya EURO 2016, Mashindano ya Mataifa ya Ulaya hapo Jana July 02, 2016.

Ujerumani ilikuwa haijawahi kuifunga Italia katika Mashindano makubwa lakini kwenye Mechi hii walistahili ushindi kwa kuwa juu kwa muda mwingi.


Miamba hiyo ya soka barani Ulaya ililazimika kwenda hadi penalti ya tisa ndipo mshindi alipopatikana kwa Italia kupoteza jumla ya penalti nne huku Ujerumani wakipoteza tatu.

Ujerumani walipata bao la kuongoza dakika ya 65 kupitia kwa Mesut Ozil lakini Leonardo Bonucci akaisawazishia Italia kwa njia ya penalti dakika ya 78. 
Mchezo huu umeweka rekodi ya kuwa na mikwaju mingi ya penati zaidi katika kipindi cha miaka 36, zimepigwa jumla ya penati 18 – mara ya mwisho kwa mchezo wa Euro kuamuliwa na idadi kama hii ya penati ilikuwa mwaka 1980 wakati Italia walipofungwa 8-9 na CzechSlovakia.

Pia Ujerumani wameendelea kuwa na rekodi nzuri ya kutopoteza mechi kwa mikwaju ya penati kwa kipindi cha miaka 40 iliyopita – historia inaonesha wamefanikiwa mikwaju mara 7 kati ya 8.

EURO 2016 ROBO FAINALI.

**Mechi zote kuanza Saa 4 Usiku Saa za Bongo

Alhamisi Juni 30,2016.

(Stade Velodrome, Marseille)

Poland 1 - 1 Portugal  [Dakika 120: 1-1, Penati: Poland 3 Portugal 5]

Ijumaa Julai 01,2016.

(Stade Pierre Mauroy, Lille)

Wales 3 - 1 Belgium 

Jumamosi Julai 02,2016.

(Stade de Bordeaux)

Germany 1 - 1 Italy  [Dakika 120: 1-1, Penati: Germany 6 Italy 5]

Jumapili Julai 03,2016.

(Stade de France, Paris)

France v Iceland

EURO 2016 NUSU FAINALI

**Mechi zote kuanza Saa 4 Usiku Saa za Bongo

Jumatano Julai 06,2016.

(Stade de Lyon)

Portugal v Wales

Alhamisi Julai 07,2016.

(Stade Velodrome, Marseille)

Germany v France/Iceland

EURO 2016 FAINALI

Jumapili Julai 10,2016.

**Saa 4 Usiku, Saa za Bongo

(Stade de France, Paris)

Portugal au Wales v Germany v France/Iceland

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad