TASAF III:-Zaidi ya milioni 200 zimetolewa Kwa kaya Masikini 7319 wilayani Biharamulo. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, June 25, 2016

TASAF III:-Zaidi ya milioni 200 zimetolewa Kwa kaya Masikini 7319 wilayani Biharamulo.

Zaidi ya  Milioni 200 zimetolewa kwa Kaya masikini sana 7319 zilizomo wilayani Biharamulo mkoani Kagera,wakati wa ruzuku iliyotolewa na TASAF III kwa awamu ya sita,ikiwa ni sawa na asilimia 90% za malengo yaliyokusudiwa.

Kiasi hicho kilitolewa kwa Walengwa waliomo kwenye mpango wa kunusuru Kaya masikini sana  unaotekerezwa na Mfuko wa maendeleo ya jamii (TA SAF III) kwa malipo ya miezi miwili ikiwa ni mwezi wa Mei na Juni mwaka huu,2016. 

Mratibu wa TASAF III wilayani Biharamulo,Bi. Beata Maganga,mbali na fedha hizo kwenda kwa walengwa,pia kiasi cha shilingi 4,269,954.55/= zimepelekwa kwenye vijiji husika,ikiwa ni kila asilimia 1.5% inayotakiwa kubaki kwa kila kijiji,lengo likiwa ni kutoa uwezesho kwa wajumbe wa serikali ya kijiji ambao wanawajibika katika majukumu ya usimamizi wa fedha za ruzuku wakati wa ugawaji ruzuku kwa walengwa.

Bi.Maganga amesema pamoja na mafanikio hayo,kiasi cha shilingi 250,504,000/= ni malipo ya ruzuku iliyotolewa kwa walengwa husika,walioko kwenye mpango.

Ametaja mafaniko yaliyopatikana kwa baadhi ya walengwa wa mpango huo tangu ruzuku hiyo ianze kutolewa Julai / Agosti mwaka jana,2015 ambavyo hadi sasa ni awamu nne,ni kuanzishwa kwa miradi midogo midogo ambavyo baadhi ya walengwa wamenunua mifugo na kuanza kufuga mbuzi,nguruwe na kuku huku wengine wakionesha kununua bati moja moja kwa ajili ya kujenga makazi mapya tofauti na ya makazi yao ya awali ambayo baadhi yao waliishi kwenye nyumba za nyasi na zilishaanza kuvuja.

Habari kwa hisani ya ITV

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad