Baadhi ya watoto wenye ulemavu wakiwa
kwenye picha ya pamoja waheshimiwa wabunge na mawaziri nje ya Ukumbi wa Pius
Msekwa mjini Dodoma.
Akisoma risala akiwawakilisha watoto
wenzake, Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Wenye Ulemavu Tanzania, Wilfred
Wilbert alisema kwanza anawashukuru FPCT kwa namna ambavyo wameweza kuwasaidia
kuwaweka pamoja, kutambua na kuzidai haki zao za msingi.
“Mabaraza ya watoto wenye ulemevu
yametuunganisha na kutupa wakati mzuri wa kujadili pamoja changamoto
zinazotukabili katika mikoa yetu, tumekuwa tukipaza sauti zetu na hata wakati
mwingine kushirikiana na viongozi mbalimbali kuwaanika wale ambao wamekuwa wakificha
watoto walemavu.
“Changamoto tunazopitia
zinazokwamisha malengo yetu ni nyingi lakini nipongeze serikali ambayo kwa
namna moja ama nyingine kupitia sauti zetu wamekuwa wakifanyia kazi mambo kama
vile miundombinu,” alisema mtoto huyo.
Naye Mhazini wa Watoto Wenye Ulemavu
Mkoa wa Tabora, Mpaji Nicolaus alipata nafasi ya kueleza changamoto
zinazowakumba ikiwa ni pamoja na ukosefu wa fedha za kuendeshea vikao vya
mabaraza na kusafirisha watoto kutoka sehemu moja hadi nyingine pamoja na vifaa
vya kutunzia ‘dokyuments’....BOFYA HAPA KUENDELEA KUSOMA HABARI HII.
|
Saturday, June 25, 2016
BUNGENI DODOMA:-Watoto wenye Ulemavu na Changamoto zao kwa Wabunge na Mawaziri.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment