KUJITOA UMOJA WA ULAYA:-Waziri mkuu wa Uingereza ajiuzulu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, June 24, 2016

KUJITOA UMOJA WA ULAYA:-Waziri mkuu wa Uingereza ajiuzulu.

Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, ametangaza atajiuzulu, baada ya kushindwa.

Waziri mkuu wa Uingereza, Bw.David Cameron, ametangaza atajiuzulu, baada ya kushindwa kuwashawishi raia wengi wa Uingereza, kusalia katika muungano wa Ulaya.

Cameron akiwa amejawa na huzuni amesema kuwa atasalia ofisini kwa siku tisini zijayo ndipo angatuke.


Bw Cameron ambaye ameongoza kampeini ya kusalia katika muungano wa EU amesema kauli hiyo imempa mshutuko mkubwa na kwa baadhi ya watu mashuhuri duniani.
Akiongea katika kikao cha waandishi wa habari nje ya afisi yake jijini London, Bw.Cameron amesema kuwa hahisi tena kuwa mtu muhimu wa kuliongoza taifa hilo kwa ufanisi chini ya uamuzi kama uliofanywa.

Sauti yake iliibua hisia hasa aliposena ..''..naipenda saana taifa hili na najihisi vizuri kuliongoza muda huo wote.

Bw.Cameron amesema kuwa kauli ya wengi sharti isikizwe japo hafahamu kwanini Waingereza walichukua uamuzi kama huo ilhali taifa hilo lilikuwa linaufanisi mkubwa sana ndani ya EU.

Bw.Cameron akiwa ameandamana na mkewe amesema bila shaka sasa utawala mpya unahitajika utakaoweza kutathmini mbinu na mkataba wa kujiondoa kutoka kwa muungano huo wa bara Ulaya.

Habari na BBC SWAHILI.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad