MAFANIKIO YETU:-Kampuni ya Bia Serengeti yazindua mradi wa maji wa 81m/- Katesh, Hanang. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, June 24, 2016

MAFANIKIO YETU:-Kampuni ya Bia Serengeti yazindua mradi wa maji wa 81m/- Katesh, Hanang.

Mmoja wa wakazi wa Kata ya Gidahababieg,Katesh akifurahia maji mara baada ya ufunguzi wa mradi wa maji uliofadhiliwa na kampuni ya bia ya serengeti katika hafla iliyofanyika siku ya jumanne June 22 wilayani Hanang, mkoa wa Manyara.

Diwani wa Kata ya Gidahababieg,Hassan Hilbagiroy akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa kata hiyo mara baada ya uzinduzi wa mradi wa maji uliofadhiliwa na kampuni ya bia ya serengeti katika hafla iliyofanyika siku ya jumanne June 22 wilayani Hanang, mkoa wa Manyara.

Pichani ni Mradi wa maji  wenye thamani ya shilingi milioni 81 mjini Katesh wilayani Hanang uliofadhiliwa na kampuni ya bia ya serengeti ikiwa ni mkakati wa kuwapatia wakazi wa eneo hilo maji safi na salama.

Juni 22, 2016- Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL)  imezindua mradi wa maji  wenye thamani ya shilingi milioni 81 mjini Katesh wilayani Hanang’ ikiwa ni mkakati wa kuwapatia wakazi wa eneo hilo maji safi na salama.

Mradi huo wenye uwezo wa kuwahudumia watu 12,000 unajumuisha kisima kilichochimbwa pamoja na mifumo yake, pampu ya maji inayotumia nishati ya jua na tenki la maji ukiwa na uwezo wa kuzalisha  lita 45,000 za maji kila baada ya saa sita.

Akizungumza latika hafla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti John Wanyancha,  alisema kuwa kisima hicho ni mkakati wa kampuni hiyo ya bia wa kuisaidia jamii chini ya mpango uitwao Maji ya Maisha na kuongeza kuwa SBL imeshatekeleza  miradi kama hiyo katika mikoa ya   Iringa, Kilimanjaro, Mwanza, Tanga, Ruvuma, Dar es Salaam, Pwani na Dodoma  ambayo imenufaisha watu zaidi ya milioni moja kwa kuwapatia maji safi na salama.

Wanyancha alisema kuwa mradi wa Katesh  sio tu kwamba utaboresha afya za wenyeji wa eneo husika bali pia utaongeza uzalishaji  kiuchumi “hususani miongoni mwa wanawake na watoto wa kike  ambao hawatalazimika kutumia saa nyingi   kutafuta maji sehemu nyingine. Hii inatoa fursa kwa watoto wa kike kuhudhuria masomo shuleni.KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad