OR-TAMISEMI
inawatangazia majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na
Vyuo vya Ufundi kwa mwaka 2016.
Wanafunzi waliochaguliwa ni kutoka shule za Serikali na zisizo za Serikali.
Jumla ya wanafunzi 65,720 wakiwemo wasichana 29,457 na wavulana 36,263
wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi.
Kati
ya wanafunzi waliochaguliwa 34,064 wakiwemo wasichana 13,466 na wavulana 20,598
sawa na asilimia 52 watajiunga na masomo ya Sayansi na Hisabati; na wanafunzi
30,897 wakiwemo wasichana 15,445 na wavulana 15,452 sawa na asilimia 47
wamechaguliwa kusoma masomo ya Sanaa na Biashara na wanafunzi 759 wakiwemo
wasichana 220 na wavulana 539 sawa na asilimia 1 wamechaguliwa kujiunga na vyuo
vya Ufundi.
Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano mwaka 2016 wataanza
muhula wa kwanza tarehe 11 Julai, 2016 na hakutakuwa na mabadiliko yoyote ya
shule.
Wanafunzi wote wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati.
Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti hadi tarehe 24 ambayo ndiyo siku ya
mwisho ya kuripoti, nafasi yake itachukuliwa na mwanafunzi mwingine aliyekosa
nafasi.
Imetolewa
na Katibu Mkuu,
OR-TAMISEMI
Tumia link hii kupata matokeo Waliochaguliwa kidato cha tano na vyuo vya
ufundi 2016.
|
No comments:
Post a Comment