KIPIGO EURO 2016:-Kocha wa Uingereza Roy Hodgson Amejiuzulu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, June 28, 2016

KIPIGO EURO 2016:-Kocha wa Uingereza Roy Hodgson Amejiuzulu.

Saa chache tu baada ya timu ya kandanda ya Uingereza kubanduliwa nje ya mashindano ya mwaka huu ya Euro 2016, Kocha wa Uingereza Roy Hodgson amejiuzulu wadhfa wake.

Hodgson alikuwa ameshuhudiwa uingereza ikiambulia kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Iceland katika mkumbo wa 16 bora huko ufaransa.

Kocha huyo mwenye umri wamiak 68 amekiongoza kikosi hicho cha Uingereza kwa miaka 4 sasa.


Hodgson alichukuwa wadhfa huo kutoka kwa kocha muitaliano Fabio Capello aliyetimuliwa kufuatia matokeo duni.

Hata hivyo kocha huyo hajakuwa na wakati mzuri kileleni mwa Uingereza, Hodgson ameiongoza Uingereza kushinda mechi tatu tu kati ya 11 alizoshiriki katika michuano mikubwa ya dunia .

Lakini kitumbua chake kiliingia mchanga baada ya Iceland - yenye jumla ya watu 330,000 - na moja kati ya timu za mataifa yaliyoorodheshwa ya chini kabisa katika orodha ya FIFA ya Ubora Duniani kwa Mataifa ya EURO 2016 ikiwa nafasi ya 34,ilipoinyuka Uingereza.

''niwieni radhi kuwa uongozi wangu wa timu hii umekomea hapo na kwa njia hii, lakini vitu kama hivi hutokea'' alisema Hodgson .

Akitangaza kujiuzulu, Hodgson alisema: “Nasikitika tumemaliza namna hii lakini haya hutokea. Natumaini mtaiona Timu ya England kwenye Fainali kubwa hivi karibuni. Sasa ni wakati wa Mtu mwingine kuongoza kundi hili la Vijana wenye njaa na vipaji vikubwa mno.”
Hodgson, ambae alishinda Mechi 33 kati ya 56 alizosimamia England, alikuwa akimaliza Mkataba wake na England mara baada ya kumalizika Mashindano haya ya EURO 2016.

Chini ya usimamizi wa Hodgson, England ilitolewa kwa Penati na Italy kwenye Robo Fainali ya EURO 2014 na kushindwa kuvuka Makundi kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Brazil.

England, ambao walifuzu Fainali za EURO 2016 wakishinda Mechi zao zote na kuwa ni Timu pekee kufanya hivyo, ilianza Fainali hizi kwenye Kundi B na kutoka Sare 1-1 na Russia, kuifunga Wales 2-1 na kisha kutoka 0-0 na Slovakia kwenye Mechi ambayo Hodgson alibadili Wachezaji 6 na kupondwa sana.

Kocha huyo aliwahi kuifunza Liverpool na West Brom. 

Nae Kepteni wa England ambae pia ni Kepteni wa Manchester United, Wayne Rooney, ameeleza: “Ni Siku ya huzuni kwetu. Siku zote kuna matokeo yasiyotegemewa kwenye Soka. Sio mbinu. Ni bahati mbaya. Tunajua sisi ni Timu nzuri. Siwezi kusimama hapa na kueleza hasa ni nini kimetokea. Mie nitabaki nikicheza. Tutaona nani mpya anakuja!”.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad