EURO 2016:-Taswira Picha Iceland ikiiondoa England kwa mabao 2-1. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, June 28, 2016

EURO 2016:-Taswira Picha Iceland ikiiondoa England kwa mabao 2-1.

Kipa wa England Joe Hart akiwa hana Furaha baada ya timu yao kufungwa magoli 2-1 na Iceland katika mchezo wa hatua ya 16 Bora Euro 2016 Uwanja wa Allianz Riviera mjini Nice, Ufaransa hapo Jana June 27, 2016 na kutolewa katika michuano hiyo.
England ilitangulia kwa bao la penalti la Nahodha Wayne Rooney dakika ya 4, kabla ya Ragnar Sigurdsson kuisawazishia Iceland dakika ya 6 na Kolbeinn Sigthorsson kufunga goli la pili dakika ya 19 huku Three Lions wakiendeleza rekodi yao ya kutoshinda mechi ya mtoano tangu Euro 2006.
Kipigo hiko kimepelekea kujiuzulu kwa kocha wa timu hiyo Roy Hodgson,ambaye ameelezea hayo mara tu bada ya kumalizika kwa mchezo huo katika mkutano na waandishi wa habari akiwa ameiongoza kwa miaka minne.

Iceland kwa sasa itakutana na mwenyeji wa michuano hiyo Ufaransa mjini Paris Jumapili Julai 3, 2016.

Katika mchezo mwingine bingwa mtetezi Hispania ameondolewa kwa kichapo cha 2-0 ilipokipiga dhidi ya Italia.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad