EURO 2016:-Ureno yafuzu robo fainali baada ya Poland na Wales ,Leo Jumapili Juni 26, ni France v Republic of Ireland, Germany v Slovakia na Hungary v Belgium. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, June 26, 2016

EURO 2016:-Ureno yafuzu robo fainali baada ya Poland na Wales ,Leo Jumapili Juni 26, ni France v Republic of Ireland, Germany v Slovakia na Hungary v Belgium.

Winga wa Ureno, Ricardo Quaresma akifunga bao pekee la ushindi kwa timu yake dakika ya 117 ikiilaza 1-0 Croatia katika mchezo wa hatua ya 16 Bora Euro 2016 usiku wa Jana June 25,2016,kwenye Uwanja wa Stade Bollaert-Delelis mjini Lens, Ufaransa na kwenda Robo Fainali .

Kwa bahati mbaya hali ya kumiliki mpira haikuisaidia Croatia badala yake,  mchezo ulifika hadi dakika 120, ndipo goli la dakika ya 3 kabla ya dakika 120 kukamilika, lilifungwa na Ricardo Quaresma  Dakika ya 117, alieingiza Mpira wavuni uliotemwa na Kipa Danijel Subasic kufuatia shuti la Cristiano Ronaldo.
Kwa ushindi huo,Ureno inakuwa timu ya tatu kufuzu robo fainali ya EURO 2016, baada ya Poland na Wales kwa kuitoa Croatia kwa Bao 1-0 katika Mechi ya Mtoano ya Timu 16 ya EURO 2016, iliyochezwa huko Stade Bollaert-Delelis Mjini Lens na kwenda Dakika 120 baada ya Sare ya 0-0 katika Dakika 90.

Kwenye Robo Fainali, Ureno watacheza na Poland ambao mapema Jana,June 25, 2016 waliitoa Switzerland kwa Penati 5-4 baada ya Sare ya 1-1 katika mchezo uliyochezwa Dakika 120.

RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16 - EURO 2016 UFARANSA.

Jumamosi Juni 25, 2016.

Switzerland 1 - 1 Poland (Baada Dakika 120 1-1, Poland yasonga Penati 5-4)

Wales 1 – 0 Northern Ireland

Croatia 0 – 0 Portugal (Baada Dakika 120, Portugal yashinda 1-0)
Jumapili Juni 26, 2016.

France v Republic of Ireland (1600, Stade de Lyon)

Germany v Slovakia (1900, Stade Pierre Mauroy, Lille)

Hungary v Belgium (2200, Stadium de Toulouse)

Jumatatu Juni 27, 2016.

Italy v Spain (1900, Stade de France, Paris)

England v Iceland (2200, Stade de Nice)

ROBO FAINALI.

Alhamisi Juni 30, 2016.

Robo Fainali ya 1, (2200, Stade Velodrome, Marseille)

Poland v Portugal

Ijumaa Julai 1, 2016.

Robo Fainali ya 2, (2200, Stade Pierre Mauroy, Lille)

Wales  v Hungary au Belgium

Jumamosi Julai 2, 2016.

Robo Fainali ya 3, (2200, Stade de Bordeaux)

Germany au Slovakia v Italy au Spain

Jumapili Julai 3, 2016.

Robo Fainali ya 4, (2200, Stade de France, Paris)

France au Republic of Ireland v England v Iceland

NUSU FAINALI.

Jumatano Julai 6, 2016.

Mshindi Robo Fainali ya 1 v Mshindi Robo Fainali ya 2 (2200, Stade de Lyon)

Poland au Portugal v Wales/Hungary au Belgium

Alhamisi Julai 7, 2016.

Mshindi Robo Fainali ya 3 v Mshindi Robo Fainali ya 4 (2200, Stade Velodrome, Marseille)

Germany au Slovakia/Italy au Spain v France au Republic of Ireland/England au Iceland

FAINALI.

Jumapili Julai 10, 2016.

(2200, Stade de France, Paris)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad