Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi wa Tanzania, Mhe.Mwigulu Nchemba amelitaka Jeshi la Polisi kutotumia nguvu kubwa katika
mambo yasiyokuwa na manufaa kwa wananchi ila nguvu hizo zitumike kupambana na
biashara ya dawa za kulevya kwa maslahi mapana ya taifa.
Waziri Nchemba ameyasema hayo
Juzi,June 24,2016, wakati akifunga mafunzo ya awali ya Polisi na Uhamiaji, katika Shule ya
Polisi Tanzania-Moshi, ambapo zaidi ya wanafunzi 3,000 walihitimu mafunzo hayo.
Alisema Polisi ikifanya
jitihada za kutokomeza biashara na matumizi ya dawa ya kulevya, kila Mtanzania
kwa kabila lake, kwa rangi yake na imani yake atalipongeza Jeshi hilo kwa kazi
ambayo watakuwa wameifanya.
Alisema Wananchi
hawataweza kulipongeza Jeshi hilo kama litatumia nguvu kubwa ya kupambana na
masuala yasiyo na tija kwa wananchi, ambapo aliwataka wahitimu wa mafunzo hayo
kutekeleza kwa vitendo yale yote waliyofundishwa kwa mujibu wa taratibu za
jeshi hilo.
Mhe.Nchemba pia ameliagiza
Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua kali za kinidhamu kwa mujibu wa taratibu za
jeshi hilo, askari Polisi wanaokiuka maadili ya utendaji kazi wao, ikiwa ni
pamoja na askari wanaobambikia watu kesi, kupokea rushwa pamoja na kukamata
raia kwa kutumia nguvu zisizostahili.
Alilaani pia tabia ya
wananchi kujichukuliwa sheria mkononi kama vile kuua watu wasiokuwa na hatia
kwa visingizio za imani za kishirikina, pamoja na sheria kutofuatwa kwa
watuhumiwa.
Mkuu wa Shule ya Polisi
Tanzania- Moshi, Matanga Mbushi, alisema wanafunzi hao wamepewa mafunzo
mbalimbali yatakayowawezesha kufanya kazi kwa ufanisi na kuongeza kuwa kati ya
wanafuzi wanaohitimu, wanafunzi 99 wametimuliwa kutokana na makosa ya nidhamu
na mimba.
|
No comments:
Post a Comment