AJALI / PICHA:-Meli ya Mizigo Yazama Unguja. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, June 26, 2016

AJALI / PICHA:-Meli ya Mizigo Yazama Unguja.

Wananchi wakishuhudia zoezi la uokoaji.

Meli ya mizigo MV.HAPPY iliyokuwa ikitoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar imezama leo,June 26, 2016,majira ya asubuhi kwenye Bahari ya Hindi eneo la Chumbe, Unguja.

Inaelezwa kuwa Meli hiyo ilikuwa imebeba Dengu gunia 450 pamoja na Mbao zaidi ya 1000 huku wafanyakazi sita waliokuwa ndani ya Meli hiyo wakiokolewa.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo ni kwamba meli hiyo ilianza kuzama majira ya saa 10 alfajiri na kufikia saa moja asubuhi ilikuwa imezama kabisa ndani ya maji.

Mpaka sasa hakuna vifo vilivyoripotiwa bali mizigo iliyokuwemo kwenye meli hiyo ndiyo iliyozama.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad