Waziri Mkuu wa Tanzania
Mhe. Kassim Majaliwa.
Akizungumza wakati wa
kuahirisha Bunge la 11 hii leo,June 30,2016, Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa,
amesema kuwa hadi kufikia Juni 30, kiasi cha tani elfu 63 za sukari zimeingizwa
kati ya tani elfu 80 zilizokuwa zinahitajika kufidia pengo lililopo.
Mhe. Majaliwa amesema
njia pekee ya kuondokana na uhabari wa sukari uliokuwepo miaka yote ni kuongeza
uzalishaji wa sukari ya ndani kwa kukamilisha mpango makakati wa maendeleo ya
sukari kwa miaka mitano ijayo.
Mhe. Majaliwa amesema
kuwa Serikali itaendelea kusimamia soko la sukari kuendelea kushuka ili mlaji
wa chini amudu kununua huku ikifanya tathmini ya mahitaji halisi ya sukari
nchini kutokana kuingiza kiasi kingi cha sukari lakini bado kumeonekana na
upungufu mkubwa.
Waziri Majaliwa amesema
moja kati ya Malengo yaliyopo katika mpango huo ni pamoja na kuanzisha kwa
viwanda vipya ambapo vitaanzishwa viwanda vya kati vitatu pamoja na kuanzisha
viwanda vikubeas katika maeneo ya Bagamoyo, Rufiji, Kigoma na Kidunda.
Aidha wataongeza tija
ya uzalishaji wa miwa inayolimwa na wakulima wadogo, kwa kuboresha upatikanaji
wa pembejeo, miundombinu ya umwagiliaji, na kuboresha mfumo wa uendeshaji wa
vyama vya wakulima wa miwa.
|
No comments:
Post a Comment