Kwaheri Bw. Nassor Mnambila.
Katika hatua nyingine Bw. Nassor
Mnambila aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera akiongea na watumishi na kuwaaga aliwashukuru kwa ushirikiano
waliompatia kwa kipindi chote alichokaa katika mkoa wa Kagera na kusema kuwa
ataendelea kuwaombea ili waendelee kutekeleza majukumu yao kikamilifu.
“Nilifika mkoani Kagera tarehe
23/12/2010 na nimeishi hapa siku 2002 nikiwa kama Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera na ninaamini kupitia nyinyi tuliweza
kufanikisha shughuli nyingi za Serikali
nawashukuru kwa ushirikiano wenu, kikubwa naomba mpatie mwenzangu
ushirikiano huo huo na mniombee afya
njema huko niendako.” Alihitimisha Bw. Mnambila.
Aidha, Bw. Fabian Gapchojiga Katibu
Tawala Msaidizi Utawala alimshukuru Bw. Mnambila kwa kazi aliyoifanya mkoani
Kagera kwa kipindi chote alichokuwa kama Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera,
kwanza, Bw. Mnambila aliukuta mkoa una watumishi 312 na ameondoka kukiwa na
watumishi 517.
Watumishi waliopandishwa vyeo kwa
wakati ni 304, aidha watumishi wengi waliweza kuendelezwa kielimu , pia Bw,
Mnambila alilishughulikia suala la Maafisa Tarafa kikamilifu mpaka wakapata
haki yao kimaslahi (Mishahara yao). Kweheri Bw. Mnambila tunakutakia kila la
kheri huko uendako na tutakumbuka daima wananchi wa Kagera. |
No comments:
Post a Comment