MATOKEO/RATIBA VPL 2015/2016:-Yanga SC yabakiza pointi nne pekee ili itangaze ubingwa wa Vodacom Tanzania bara. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, May 03, 2016

MATOKEO/RATIBA VPL 2015/2016:-Yanga SC yabakiza pointi nne pekee ili itangaze ubingwa wa Vodacom Tanzania bara.

Klabu ya soka ya Yanga SC imezidi kuusogelea ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu kuafutia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Stand United jioni ya leo,May 03,2016 Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Ushindi huo ulitokana na mabao mawili ya washambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe, Donald Ngoma na Amissi Tambwe wa Burundi, unaifanya Yanga ifikishe pointi 68 baada ya kucheza mechi 27.

Yanga SC sasa imebakiza pointi nne pekee ili itangaze ubingwa wa Vodacom Tanzania bara kwa msimu huu wa 2015-2016.

Stand United walipata goli la kwa mkwaju wa penati uliokwamishwa wavuni na Elius Maguri dakika ya 81 kipindi cha pili baada ya Thabani Kamusoko kumuangusha mchezaji wa Stand kwenye box.

Bao hilo la Maguri ni la 12 kwenye ligi msimu huu.

Matokeo hayo yanaifanya Yanga SC indelee kujichimbia kwenye kilele cha Ligi huku ikihitaji pointi nne tu kutetea ubingwa wake.

Yanga SC sasa imefikisha pointi 68, kama itapata pointi nne itafikisha jumla ya pointi 72 ambazo haziwezi kufikiwa na Azam FC wala Simba SC hata kama zitashinda michezo yao yote minne iliyosalia ambazo.

Azam FC inapointi 59, ikishinda mechi zake zote nne itafikisha jumla ya pointi 71, Simba SC pia ina pointi 58 na ikishinda mechi zake zote zote itafikisha pointi 70 na kuiacha Yanga ikitwaa taji hilo kwa mara nyingine tena.

Ligi hiyo kuu soka Tanzania bara itaendelea tena hapo kesho Jumatano Mei 4, 2016 Azam FC ya Dar es Salaam itakuwa mwenyeji wa JKT Ruvu ya Pwani kwenye Uwanja wa Azam, Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad