TFF HAITATANGAZA MSHINDI WA STARTIMES KUNDI C:-Ni baada ya 8-0 na 7-0 za Leo February 13,2106. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, February 13, 2016

TFF HAITATANGAZA MSHINDI WA STARTIMES KUNDI C:-Ni baada ya 8-0 na 7-0 za Leo February 13,2106.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) halitatangaza timu iliyopanda Ligi Kuu msimu ujao 2016/2017 kutoka Kundi C, mpaka itakapoamuliwa na vyombo husika vya TFF baada ya michezo ya kundi hilo kuchezwa leo,February 13,2016 jioni katika viwanja tofauti nchini.

TFF imefikia hatua hiyo ili kupata nafasi ya kupitia taarifa za michezo kati ya JKT Kanembwa v Geita Gold na Polisi Tabora v JKT Oljoro iliyochezwa leo jioni katika mikoa ya Kigoma na Tabora.

Taarifa za michezo hiyo kutoka kwa wasimamizi husika na vyanzo vingine vinakusanywa ili zifanyiwe kazi na vyombo husika vya TFF.

Katika michezo hiyo ya leo, Geita iliibuka na ushindi wa mbao 8 – 0 dhidi ya JKT Kanembwa, huku Polisi Tabora wakiibuka na ushindi wa mabao 7 – 0 dhidi ya JKT Oljoro.

IMETOLEWA NA TFF

Matokeo.

Jumamosi Februari 13,2016.

Kundi B

Kimondo FC  2 - 0 Kurugenzi FC    

Njombe Mji 2 - 0 Lipuli FC

Ruvu Shooting 0 – 0 Polisi Morogoro

Burkinafaso FC 2- 3 JKT Mlale

Kundi C

Mbao FC 1 – 1 Polisi Mara       

Polisi Tabora  7 – 0 JKT Oljoro

JKT Kanembwa 0 – 8 Geita Gold FC


Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari  kwa WhatsApp +255789925630  Or  +255756830214.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad