![]() |
Dkt. Shein
alisema kuwa CCM ilizaliwa mwaka 1977 baada ya kuungana kwa vyama viwili vya
ukombozi vikiwemo TANU na Afro shraz party (ASP) ambapo chama hicho kimeweza
kupigania haki za wanyonge kwa kusimasmisha serikali zenye misingi imara ya
kuwatumikia wananchi kwa moyo wote bila ya ubaguzi.
“ Serikali
nyingi zilizoundwa na vyama vya ukombozi duniani zimeangushwa na wakoloni kwa
njia za kitapeli lakini sisi serikali zetu bado ni imara na zitaendelea
kutawala wananchi kwa njia bora na za kidemokrasia.
"Pia ni
lazima tuendelee kujitathimini kwa kila jambo nje na ndani ya chama chetu kwani
bado kuna changamoto mbali mbali zinazotakiwa kufanyiwa kazi ipasavyo”, alisema
Dkt. Shein.
|
![]() |
Aidha Dkt.
Shein aliwasihi wafuasi wa chama hicho na wananchi kwa ujumla kujitokeza kwa
wingi katika uchaguzi wa marudio utakaofanyika Machi 20 mwaka huu, ili
wapatikane viongozi wa kuongoza dola kwa mniaka mitano ijayo.
Dkt.Shein
alifafanua kwamba msingi wa uchaguzi wa marudio upo kikatiba kwani uchaguzi
mkuu uliopita ulifutwa kisheria na mamlaka iliyokuwa inahusika na usimamizi na
uratibu wa uchaguzi huo baada ya kubaini kasoro.
|
![]() |
Akizungumzia
mgogoro wa kisiasa uliopo visiwani Zanzibar, Dkt. Shein alisema kuwa ulikuwa
utatuliwe kwa njia za mazungumzo lakini kiongozi wa CUF ambaye ni Maalim Seif
Sharif Hamad aliyeomba mazungumzo ya maridhiano kabla hayajamalizika yeye
alienda kutoa siri za vikao kwa waandishi wa habari Dar es saalam na baadae
kuandika barua ya kujitoa katika mazungumzo hayo.
Aidha
aliwataka wananchi kuendelea kulinda Amani na utulivu wa nchi na kuepuka
kutumiwa na baadhi ya vyama vya kisiasa kufanya vurugu sizisokuwa na msingi kwa
maslahi ya nchi.
Akizungumza
katika hafla hiyo Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alisema kuwa
Zanzibar CCM itaendelea kuwa chama cha wananchi wote kinachoongozwa na
uzalendo.
Alisema kuwa
mpaka sasa CCM Zanzibar imejiandaa kwa kila hatua katika kushiriki kwenye
uchaguzi wa marudio utakaofanyika Machi 20 mwaka huu.
|
No comments:
Post a Comment