Ni mtoto
mdogo alie na umri wa Miaka 16, mkazi wa Maduka Tisa Ilemela Mkoani Mwanza
(Kushoto). Mwaka 2013 alihitimu darasa la saba lakini alishindwa kujiunga na
Kidato cha kwanza kutokana na ugumu wa maisha licha ya kwamba alifaulu kwenda
kidato cha kwanza.
"Baba
aliachana na mama na kwa kuwa mama anaumwa niliamua kuja hapa (Jijini Mwanza)
kwa ajili ya kutafuta pesa ya kutumia nyumbani (anajishughulisha na biashara ya
machinga). Kidogo ninachokipata napeleka nyumbani kwa ajili ya matumizi. Lakini
kwa sasa hali inazidi kuwa ngumu maana mgambo wa Jiji wanatusumbua sana".
Anasema mtoto huyo ambae alidokeza kuwa ana ndoto za kuwa mmoja wa wafanyabiashara
wakubwa nchini.
|
Mmoja wa
wakazi wa Jiji la Mwanza (Kulia) anasema wazazi wanapotengana wanasababisha
ongezeko kubwa la watoto mitaani na hata wakati mwingine idadi ya akina mama
wanaoomba omba mtaani inaongezeka.
Anasema kama
migogoro ya kifamilia haitakomeshwa, idadi ya watoto mitaani pamoja na akina
mama kutanda barabarani maeneo ya mjini wakiomba pesa kutoka kwa wasamalia wema
itazidi kushuhudiwa ikiongezeka kila kukicha.
Imeandaliwa
na George Binagi wa Binagi Media Group.
|
No comments:
Post a Comment