LIGI KUU VODACOM 2015/2016:-Yanga SC wameidunda Simba SC 2-0 Na Matokeo Mengine ya Leo February 20,2016. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, February 21, 2016

LIGI KUU VODACOM 2015/2016:-Yanga SC wameidunda Simba SC 2-0 Na Matokeo Mengine ya Leo February 20,2016.


Wachezaji wa Yanga wakiongozwa na Simon Msuva (katikati) wakishangilia ushindi wao wa bao 2-0 dhidi ya Simba kwenye mchezo wa Dar Derby uliopigwa kwenye uwanja wa taifa February 20, 2016
Wachezaji wa Yanga SC wakiongozwa na Simon Msuva (katikati) wakishangilia ushindi wao wa bao 2-0 dhidi ya Simba SC kwenye mchezo wa Dar Derby uliopigwa kwenye uwanja wa taifa February 20, 2016.

Yanga SC imefuta rekodi ya kocha Jackson Mayanja ya ushindi mfululizo baada ya kupata ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Simba SC mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliozikutanisha timu hizo kwenye mchezo wa marudiano.

Ushindi huo ni wa pili kwa Yanga SC dhidi ya Simba SC ndani ya msimu huu wa 2025-2016 baada ya awali kupata ushindi kama huo kwenye mchezo wa raundi ya kwanza.

Beki wa kushoto wa Simba SC Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ akimtoka beki wa kulia wa Yanga Juma Abdul
Beki wa kushoto wa Simba SC Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ akimtoka beki wa kulia wa Yanga Juma Abdul

Bao la kwanza la Yanga SC limefungwa na Donald Ngoma dakika ya 39 baada ya Hassan Kessy kutoa pasi fupi kwa golikipa wake Vicent Agban ambayo ilinaswa na mzimbabwe huyo na kuwekwa kambani mapema kipindi cha kwanza.

Yanga walipata bao la pili kutoka kwa nyota wa mchezaji wa zamani wa Simba Amis Tambwe dakika ya 72 kipindi cha pili.
Adbi Banda akiwaungia mkono mashabiki wa Simba mara bada ya kutolewa nje ya mchezo kwa kadi nyekundu na mwamuzi Jonesi Rukyaa kufuatia kuoneshwa kadi mbili za njano
Adbi Banda akiwaungia mkono mashabiki wa Simba mara bada ya kutolewa nje ya mchezo kwa kadi nyekundu na mwamuzi Jonesi Rukyaa kufuatia kuoneshwa kadi mbili za njano.

Rekodi unazotakiwa kujua

    Yanga SC ndiyo timu ya kwanza kuifunga Simba tangu iwe chini ya kocha Jackson Mayanja tangu kocha huyo atangazwe kuchukua mikoba ya Dylan Kerr.

    Simba SC ilikuwa haijafungwa zaidi ya goli moja tangu iwe chini ya Mayanja, Yanga wamekuwa timu ya kwanza kuifunga Simba zaidi ya goli moja baada ya kuifunga bao 2-0.
Raha ya ushindi, mashabiki wa Yanga wakishangilia ushindi wao wa bao 2-0 dhisi ya Simba
Raha ya ushindi, mashabiki wa Yanga wakishangilia ushindi wao wa bao 2-0 dhisi ya Simba SC.

    Yanga SC inapanda kileleni mwa ligi kwa mara nyingine baada ya kufikisha pointi 46 ikiwa imecheza michezo 19 huku Simba SC yenye pointi 45 sawa na Azam FC ikishuka hadi nafasi ya tatu ikitofautiana kwa wastani wa magoli na Azam  FC.
Mashabiki wa Yanga waksaidia kumshusha shabiki mwenzao aliyepoteza fahamu ili apatiwe huduma ya kwanza
Raha ya ushindi, mashabiki wa Yanga SC wakishangilia ushindi wao wa bao 2-0 dhisi ya Simba SC.

    Yanga SC inapanda kileleni mwa ligi kwa mara nyingine baada ya kufikisha pointi 46 ikiwa imecheza michezo 19 huku Simba SC yenye pointi 45 sawa na Azam FC ikishuka hadi nafasi ya tatu ikitofautiana kwa wastani wa magoli na Azam  FC.
Mashabiki wa Simba wakiwa wametulia jukwaani baada ya kupigwa bao mbili na watani zao wa jadi Yanga
Mashabiki wa Simba SC wakiwa wametulia jukwaani baada ya kupigwa bao mbili na watani zao wa jadi Yanga SC

Simba SC itakuwa mwenyeji wa Mbeya City March 6, 2016 kwenye mchezo wao ujao wa VPL 2015/2016  kwenye uwanja wa taifa.

Yanga SC wataialika Mtibwa Sugar kwenye mchezo unaofuata katika liga, mchezo huo utapigwa kwenye uwanja wa taifa February 24, 2016.

Matokeo ya michezo mingine iliyopigwa leo kwenye viwanja mbalimbali

Mgambo JKT 1-1 Tanzania Prisons

Stand United 1-1 JKT Ruvu

Mbeya City 0-3 Azam FC

Toto Africans 1-1 Kagera Sugar


Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari  kwa WhatsApp +255789925630  Or  +255756830214.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad