VPL 2015/2016:-Simba SC na Azam FC zashinda pia kuna matokeo ya michezo mingine iliyohezwa leo January 20,2016. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, January 20, 2016

VPL 2015/2016:-Simba SC na Azam FC zashinda pia kuna matokeo ya michezo mingine iliyohezwa leo January 20,2016.

Daniel Lyanga (jezi namba 10) akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kuifungia Simba bao la pili kwenye mchezo dhidi ya JKT Ruvu

Simba SC  wamepata ushindi wao wa pili mfululizo chini ya Kocha wao mpya Jackson Mayanja walipoichapa JKT Ruvu 2-0 kwa Penati ya Hamisi Kiiza na Goli la Lyanga huku Goli zote zikifungwa Kipindi cha Pili cha  mchezo huo wa Ligi kuu uliochezwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam leo Jumatano January 20,2016.
Ushindi wa leo unaifanya Simba SC kufikisha pointi 33 nyuma ya mahasimu wao Yanga SC bado wanapointi zao 36 huku wakisubiri kucheza mechi yao ya kesho Al hamis January 21,2016 dhidi ya Majimaji wakati Azam FC yenye pointi 39 inakaa kileleni mwa ligi baada ya ushindi wa leo wa Bao 2 -1 dhidi ya Mgambo JKT uliochezwa jijini Tanga.

Endapo Yanga SC wakishinda mchezo wao wa kesho watafikisha pointi 39 sawa na Azam FC na kuongoza tena ligi kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa. Lakini kama watatoka sare au watafungwa basi watawaachia Azam usukani wa kuongoza ligi.

Leo January 20, 2016 imepigwa jumla ya michezo mitatu ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania Tanzania bara 2015/2016 kwenye viwanja  vya miji tofauti.

Hapa chini kuna matokeo ya michezo mingine iliyohezwa leo January 20,2016.

Mgambo JKT 1 - 2 Azam FC (Mkwakwani Stadium-Tanga)

Ndanda FC 4 - 1 Mbeya City (Nangwanda Sijaona-Mtwara)

Standa United 2 - 1 Toto Africans (Kambarage Stadium-Shinyanga)

Tanzania Prisons 2 - 1 Coastal Union (Sokoine Stadium-Mbeya)

Kesho itapigwa michezo mingine mitatu kwa ajili ya kukamilisha duru la kwanza la ligi kuu Tanzania bara ambapo mechi hizo zitakamilisha mechi 15 za kwanza za ligi msimu huu kisha kupisha ratiba ya michuano ya FA kisha kuanza kupigwa michezo mingine ya lala salama ya ligi hiyo.

LIGI KUU VODACOM 2015/2016

Ratiba.

Alhamisi Januari 21,2016.

Mwadui FC v Kagera Sugar 

African Sports v Mtibwa Sugar

Yanga SC v Majimaji

Jumamosi Januari 22,2016.

Coastal Union v Yanga SC

Simba SC v African Sports

JKT Ruvu v Majimaji

Tanzania Prisons v Azam FC 

Mtibwa Sugar v Stand United

Mwadui FC v Toto Africans


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp  .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad