Stoke
walipopanda daraja msimu wa 2008/09 – Manchester United waliwafunga 1-0 @Britannia kisha wakaenda kutwaa ubingwa
wa msimu huo.
Msimu
uliofuatia – mabingwa walikuwa Chelsea na walipata matokeo ya 2-1 dhidi ya
Stoke @Britannia – United walipochukua ubingwa msimu wa 2010/11 waliwafunga
2-1.
City
walipata sare ya 1-1 dhidi ya Stoke @Britannia katika msimu waliochukua ubingwa
wao wa kwanza wa EPL mwaka 2012, na msimu uliofuatia United wakashinda 2-0.
History
ilijirudia tena misimu miwili iliyopita wakati City walipopata sare tasa
@Britannia na wakaenda kutwaa ubingwa, kabla ya Chelsea kurudi London na
ushindi wa 2-0 kabla ya kwenda kutwaa ubingwa msimu uliopita.
|
Msimu huu
Leicester wamepata sare ya 2-2 na jana usiku Gunners wakapata sare ya 0-0 –
hivyo mpaka sasa ni vilabu hivyo tu ambavyo vimepata matokeo chanya katika
dimba la Britannia.
Kwa wale
wazee wa KuBET – mnaweza kuanza kuwawekea mizigo Leceister, Arsenal na labda
Tottenham kwamba wanaweza kutwaa ubingwa wa EPL.Kwa hisani ya shaffihdauda.
|
No comments:
Post a Comment