|
Msafara wa
magari uliokuwa umembeba Mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika wa
Wachezaji wa Ndani 2015, Mbwana Samata,ulionaswa na Camera ya Globu ya jamii
maeneo ya Morocco jana,January 09,2016 jioni ukitokea hoteli ya Kempinsk baada ya kuzungumza na
vyombo vya habari,Msafara huo akiwemo Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na
Michezo Mh.Nape Nnauye ulipita maeneo kadhaa ya jiji la Dar na kukomea katika
kiota cha Escape One Mikocheni jijini Dar,ambako alikutana na kupongezwa na
Wadau mbalimbali wa tasnia ya Michezo.Mwanasoka huyo aliwasili juzi,Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam
akitokea Abuja, Nigeria katika hafla ya utoaji tuzo kwa
mwanamichezo
bora.
PICHA NA
MICHUZI JR-MMG.
|
No comments:
Post a Comment