Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewasimamisha kazi
Kamishna Mkuu wa Uhamiaji Bwana Sylvester Ambokile na Kamishna wa Uhamiaji
anayeshughulikia Utawala na fedha Bwana Piniel Mgonja ili kupisha uchunguzi, kufuatia dosari
alizozibaini Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mheshimiwa Charles Kitwanga
alipotembelea Idara ya Uhamiaji hivi karibuni.
Katibu Mkuu
Kiongozi , Balozi Ombeni Sefue amezitaja dosari hizo kuwa ni pamoja na tuhuma za
rushwa, ukusanyaji mbaya wa maduhuli ya serikali, ukiukwaji wa taratibu za
manunuzi na utendaji mbovu.
Balozi Sefue
amesema watendaji hao wakuu wa Uhamiaji wamesimamishwa kazi mara moja hadi hapo
uchunguzi utakapokamilika na kwamba endapo watabainika kutokuwa na makosa Rais
ataamua hatma yao.
Katika Hatua
nyingine Rais John Pombe Magufuli amemrejesha Bwana Eliakim Chacha Maswi kuwa
Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, baada ya kukamilisha kazi maalum aliyomtuma
kuifanya katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Kabla ya
kurejeshwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Bwana Maswi aliteuliwa kuwa
Kaimu Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema, Rais Magufuli amefanya mabadiliko hayo
kwa lengo la kumtafuta mtu mwenye utaalamu wa kuendeleza kazi iliyofanywa na
Bwana Maswi.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es
salaam
20 Januari,
2016
>>>>Msikilize
Katibu Mkuu Kiongozi Akiongea..
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii,
Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha
kwa WhatsApp +255789925630 .
|
No comments:
Post a Comment